Manchester
City watakuwa na kibarua kizito mbele ya Barcelona katika mechi za mtoano
hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Arsenal
wenyewe watakuwa na kazi nzito mbele ya bingwa mtetezi Bayern Munich ikiwa ni
marudiano ya hatua hiyo ya msimu uliopita.
Kocha Arsene
Wenger alisema “Katika miaka minne au mitano iliyopita tumekuwa na wakati mgumu
kila tunapoingia kwenye hatua hii, labda wakati huu tutakuwa na bahati.”
Chelsea
mabingwa wa 2012 wenyewe wametupwa kwa Galatasaray wakati mabingwa wa
England, Manchester United watajiuliza upya mbele ya Olympiakos ya
Ugiriki.
Michezo
mingine ya hatua hiyo itawakutanisha mabingwa mara saba AC Milan dhidi ya Atletico
Madrid, Bayer Leverkusen dhidi ya Paris St-Germain, Schalke wametupwa kwa Real
Madrid na Zenit St Petersburg wataonyeshana kazi na Borussia Dortmund.
City
iliichapa Bayern Munich 3-2 katika mchezo wa mwisho wa Kundi D wangeweza
kumaliza vinara wa kundi hilo kama wangeshinda 4-2.
Kocha wa
Manuel Pellegrini hana wasiwasi sana na Barcelona ya sasa, lakini anajua kwamba
anakazi kubwa ya kufanya kuhakikisha Manchester City wanarudia katika upangwaji
wa ratiba nyingine hapo Machi jijini Nyon.
Mkurugenzi
wa City, Ferran Soriano na mkurugenzi wa ufundi, Txiki Begiristain wote
wamefanya kazi Barcelona na ndio waliomuuza Yaya Toure kwa City 2010.
Arsenal
iliifunga Bayern Munich 2-0 mwezi Machi, lakini waliondolewa kwa sheria ya bao
la ugenini msimu uliopita katika robo fainali baada ya kunyukwa 3-1 kwenye
mchezo wa kwanza.
Bayern pia
imeiondoa Gunners kwenye mashindano hayo mara mbili kila walipokutana kwenye
hatua ya mtoano.
Mechi ya
kwanza ya 16 bora zitachezwa kati ya Februari 18 na 19 kwa vinara wa makundi
yote kuwa nyumbani wakati mechi za marudiano zitafanyika Februari 25 na 26.
No comments:
Post a Comment