Hii ndio taswira ya Sanamu ya Rais wa kwanza mweusi iliyozinduliwa rasmi jijini Pretoria,Africa ya Kusini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, December 17, 2013

Hii ndio taswira ya Sanamu ya Rais wa kwanza mweusi iliyozinduliwa rasmi jijini Pretoria,Africa ya Kusini.

Nchi ya Afrika kusini imezindua Jumatatu hii(Desemba 16,203) sanamu mpya ya Rais wa kwanza mweusi wa taifa hilo aliye zikwa Jumapili (Desemba 15,2013) Mzee Nelson Madiba Mandela mjini Pretoria, kwenye eneo la Union Bulding, jengo ambalo lilitumika kumuapisha Mandela Mwaka 1994 kuwa rais wa Afrika kusini.



Uzinduzi huo unafanyika siku moja baada ya mwili wa Nelson Mandela kuzikwa katika kijiji cha Qunu, imezinduliwa kumbukumbu nyingine ambayo ni sanamu kubwa yenye futi 30 iliyopewa jina la Nelson Mandela Unity Statue.

Rais wa Afrika ya kusini, Bw.Jacob Zuma, amewaongoza viongozi mbali mbali wa serikalini na familia ya Nelson Mandela kuzindua rasmi sanamu hiyo mpya ya Mandela ambayo inatajwa kuwa kubwa zaidi duniani, na itakua na urefu wa zaidi ya mita 9.
 
Wakati akizindua sanamu hiyo jana(Desemba 16,2013), Rais Zuma alisema kwamba sanamu nyingi za Mandela zinamuonyesha akinyoosha mkono wake mmoja juu kama ishara ya mapambano iliyokuwa ikitumiwa na Chama cha ANC.
Uzinduzi wa sanamu hiyo umeenda sambamba na siku maalumu ya  upatanishi, kukumbuka tukio la mwaka 1838 ambapo jeshi la Voortrekkers lilipigana na kulishinda jeshi la jamii ya Wazulu.

Katika vita hivyo, watu zaidi ya 100 walipoteza maisha, na baadae jeshi hilo liliondoka kwenye ardhi ya watu kutoka jamii ya Wazulu.

Tukio la pili kwa tarehe hii ya leo ni lile la mwaka 1961, wakati chama cha ANC kiliunda jeshi lake ambalo lilijulikana kwa jina la Umkhonto we Sizwe dhidi ya utawala wa Frederik de Klerk kwa kukabiiana na ubaguzi wa rangi.

Siku hii ya mapumziko nchni Afrika ya kusini ilitangazwa rasmi na Nelson Madiba Mandela, baada ya kutangazwa kua rais wa Afrika ya kusini tarehe 10 may 1994.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad