Hatimaye Mwili wa Hayati Nelson Mandela wapumzishwa katika nyumba ya milele kijijini cha Qunu . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 15, 2013

Hatimaye Mwili wa Hayati Nelson Mandela wapumzishwa katika nyumba ya milele kijijini cha Qunu .


Hatimaye mwili wa Rais wa kwanza mzalendo nchini Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela umezikwa leo(Desemba 15,2013) jumapili katika kijiji cha Qunu mkoa wa Eastern Cape, mazishi hayo yanatamatisha juma moja la maombolezo ya shujaa huyo wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi.


Watu wapatao 4,500 wakiwemo wawakilishi wa mataifa mbalimbali wamehudhuria mazishi hayo.



Mandela aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95 baada ya kusumbuliwa na maradhi ya mapafu kwa muda mrefu, amepumzishwa kwa amani kwa misingi ya tamaduni na mila za watu wa ukoo wake wa Xhosa aba Thembu.


 



"Kamera hazikuruhusiwa wakati wa mazishi, familia haikutaka watu waone maiti ilipoteremshwa kaburini," wala Vyombo vya habari na wageni wa hishima hawakuweza kuhudhuria pia.


"Jumapili baada ya mwili wake kuwekwa katika kaburi lake, taratibu zote za kimila zitafanywa na Himaya ya Kifalme," na kwa mujibu wa  Kiongozi wa Jamii ya Xhosa, Nokuzola Mndende anasema"Zitakuwa ni mila na desturi za jadi,kwa Fahali (ng'ombe dume) kuchinjwa kwa ajili ya kumsindikiza, na ni familia ya Mandela pekee watakaohusika na taratibu hizi za kumwandalia safari njema."


Akihutubia maelfu ya watu waliofika kuhudhuria mazishi ya Mandela, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewataka wananchi wake kuendeleza urithi mwema walioachiwa na kiongozi huyo.

Watu mbalimbali waliopata fursa ya kuhutubia waombolezaji wameeleza wasifu wa kiongozi huyo, huku Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akibainisha jinsi uhusiano baina ya Mataifa hayo mawili ulivyoimarishwa na waasisi wa Mataifa hayo, Hayati Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mandela ambao kwa pamoja wanakumbukwa kwa harakati zao katika historia ya ukombozi barani Afrika.



"Kamera hazikuruhusiwa wakati wa mazishi, familia haikutaka watu waone maiti ilipoteremshwa kaburini," wala Vyombo vya habari na wageni wa hishima hawakuweza kuhudhuria pia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad