![]() |
Mazishi ya
Nelson Mandela yanaendelea leo (Desemba 15,2013) katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Eastern Cape
na kumaliza wiki moja ya maombolezi ya shujaa wa Afrika mwendazake Nelson
Mandela.
|
![]() |
Wanajeshi
hawa walisindikiza jeneza la Mandela hadi katika ukumbi maalum ambako ibada ya
kumuaga Mandela ilifanyika .
|
![]() |
Waliokuwa
wake za Mandela walikesha usiku kucha kabla mazishi kufanyika leo()Desemba
15,2013).
|
![]() |
Ngozi
iliyofunikwa jeneza la Mandela kama ishara ya umuhimu wa Mandela katika jamii
ya watu wa Thembu.
|
![]() |
Kuambatana
na tamaduni za watu wa Thembu ukoo wa Mandela, jeneza la mfu hufunikwa kwa
ngozi ya Ng'ombe ishara ya umuhimu wake katika jamii.
|
![]() |
Wageni
mashuhuri walifika hapa kumuaga Mandela akiwemo Oprah Winfrey na Richard
Branson na wengi wangineo.
|
Takriban
watu 4,500 ikiwemo wageni wa kimataifa wanahudhuria mazishi hayo ambayo ni ya
mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa.
Familia ya
Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi ya leo huku kukiwa na muimbaji ambaye
atakuwa anaita mizimu ya mababu wa kale na pia wakiongelesha mwili wa Mandela
kumwambia kuwa sasa anazikwa.
Ni kuambatana na tamaduni na mila za watu wa ukoo
wa Mandela wa Thembu
No comments:
Post a Comment