Aliyekuwa
mgombea Ubunge Jimbo la Ngara mkoani Kagera,kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
katika uchaguzi mkuu uliopita 2010 ,Dk. Peter Bujari ametangaza rasmi kukihama
chama chake na kujiunga na chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Akizungumza
na wandishi wa habari nyumbani kwake katika kijiji cha Bikiriro wilayani
Ngara,Dk Bujari alisema ameamua kujiunga na CHADEMA baada ya kuridhishwa na
sera na uwajibikaji ndani ya chama hicho.
Alisema kuwa
atakabidhi kadi ya CCM kwa Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Bw. Freeman Mbowe ambaye
anatarajiwa kuwa wilayani Ngara Jumamosi Disemba 28 mwaka huu.
Awali
taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Bw.
Stanford Kennedy Festo zililidokeza kuwa
Dk. Bujari alikuwa na mpango wa kuhamia CHADEMA na kwamba suala hilo
lingetangazwa rasmi baadae.
Hata hivyo
alisema kuondoka kwake CCM na kwenda CHADEMA ni kutaka kuleta mabadiliko katika
upinzani dhidi ya Chama cha Mapinduzi, na kwamba atahakikisha kuwa wafuasi
aliokuwa nao wanahamia kwenye chama hicho.
Dk Bujari
alisema Chama cha Mapinduzi CCM kina muda mrefu tangu kuanzishwa kwake lakini
kimeshindwa kuwajibika na kuwaletea maendeleo wananchi hali ambayo yeye kama
mzalendo hawezi kuivumilia.
Dk Peter
Bujari alijiunga na CCM mwaka 1995 na amekuwa akijuhusisha na utoaji wa huduma
za kijamii hasa elimu na afya katika wilaya ya Ngara kupitia shirika lake la
HUMAN DEVELOPMENT TRUST (HDT) ambapo amesaidia kuhamasisha jamii kuondokana na
magonjwa ya malaria na kusaidia jamii
zenye uwezo duni.
Pamoja na
jitihada zake ametoa msaada kwa watoto yatima kuwaendeleza kielimu katika
wilaya za Ngara na Biharamulo huku baadhi ya familia zikipewa mitaji ya fedha
ama mifugo (mbuzi kuendeleza maisha na kuongeza kipato cha familia.
Mwaka 2010
alikuwa kwenye orodha ya wanachama 10 wa
CCM waliowania nafasi ya ubunge kwenye jimbo la uchaguzi la Ngara ambapo
wanachama walimpa kura 2713 na aliyepata
nafasi hiyo ni Mbunge wa sasa kupitia chama hicho Deogratias Ntukamazina
aliyepata kura 4900 za wanachama wa CCM.
Source:-Ngara kwetu blog.
No comments:
Post a Comment