Ziko 9 na kubakia 7 ambazo zitacheza Fainali za CHAN mwaka 2014 huko nchini Afrika Kusini kuanzia Januari 10. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 28, 2013

Ziko 9 na kubakia 7 ambazo zitacheza Fainali za CHAN mwaka 2014 huko nchini Afrika Kusini kuanzia Januari 10.

Wachezaji wa timu ya taifa 'Taifa Stars' na Uganda Cranes wakiingia uwanjani tayari kwa kuanza mechi yao ya kufuzu kucheza Chan iliyofanyika kwenye uwanja wa
Mandela, Namboole mjini Kampala.


 Kikosi cha Stars kilipangwa hivi; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, David Luhende/Vincent Barnabas, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Frank Domayo/Simon Msuva, Salum Abubakar, John Bocco/Haruni Chanongo, Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.


Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imerejea nyumbani  leo (Julai 28 mwaka huu) saa 4 usiku kwa ndege ya PrecisionAir.

Kikosi cha timu ya taifa ya Uganda 'Uganda Cranes' ndicho kilichoiburuza Taifa Starz na kwa mabao 3-1 na hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 4-1.

Mchezaji wa Taifa Stars Aggrey Morris (katikati) akiwania mpira huku akizongwa na mabeki wa Uganda Cranes.Taifa Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

Amri Kiemba akipongezwa na Mrisho Ngasa/ Aboubakar Salum 'Sure Boy' baada ya kushinda bao la kusawazisha dhidi ya Uganda Cranes.

Washabiki wa Taifa Stars wakishangilia goli la kusawazisha. Lililofungwa na...Amri Kiemba dhidi ya Uganda Cranes.

Amri Kiemba dhidi ya Uganda Cranes.


Mchezo uwanjani kati ya  Uganda 'Uganda Cranes'  dhidi ya  Taifa Starz na Starz kufungwa  mabao 3-1 na hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 4-1 katika kuwania  kufuzu Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) kwa mara ya pili mfululizo .

Timu ambazo zitacheza Fainali za CHAN  mwaka 2014 huko nchini  Afrika Kusini kuanzia Januari 10 Mwakani zimefikia 9 na kubakia 7, baada ya Timu kadhaa kufuzu jana Jumamosi (Julai 27,2013) .

Leo (Julai 28,2013), Timu nyingine 3 zitafuzu na Congo-Brazzaville, Mali na Sudan zipo kwenye nafasi nzuri kuchukua nafasi hizo wakati Sudan wakirudiana na Burundi huko Khartoum baada ya kutoka sare 1-1 katika Mechi ya kwanza, Congo wakirudiana na Congo DR huku Mali, walioshinda Mechi ya kwanza 3-1, wakicheza ugenini na Guinea.

Zambia noa wapo kwenye hali nzuri kutinga Fainali baada ya Jana kutoka Sare ugenini ya Bao 1-1 na Botswana.


Timu zilizofuzu hapo Jana :-


-South Africa [Wenyeji]

-Libya

-Morocco

-Mauritania

-Ghana

-Nigeria

-Burkina Faso

-Ethiopia

-Uganda


Tanzania (Taifa Stars) ilishindwa kufuzu Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) kwa mara ya pili mfululizo baada ya jana (Julai 27 mwaka huu) kufungwa mabao 3-1 na Uganda Cranes, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 4-1.

Stars ambayo ilicheza fainali za kwanza zilizofanyika Ivory Coast mwaka 2009 ilimaliza kipindi cha kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Kampala ikiwa sare ya bao 1-1.

Wenyeji ndiyo walioanza kufunga bao dakika ya saba katika mechi hiyo iliyochezeshwa na Kanoso Abdoul Ohabee kutoka Madagascar.

Frank Kalanda alifunga bao hilo akimalizia mpira uliopigwa ndani ya eneo la hatari la Tanzania.

Bao hilo halikuonekana kuichangaza Taifa Stars, kwani ilitulia na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 18 mfungaji akiwa Amri Kiemba kutokana na pasi nzuri ya Mrisho Ngasa kwenye kona ya eneo la mita 18.

Dakika ya 32 nusura Taifa Stars ipate bao, lakini mkwaju maridadi wa Mrisho Ngasa ambao tayari ulikuwa umempira kipa HAmza Muwonge uligonga mwamba kabla ya kuokolewa na mabeki wa Uganda Cranes.


Mabao mengine ya Uganda Cranes yalifungwa dakika ya 48 kupitia kwa Brian Majwega na lingine dakika ya 63 mfungaji akiwa tenda Kalanda kutokana na makosa ya Salum Abubakar kupokonywa mpira wakati akiwa katika nafasi nzuri ya kutoa pasi kwa mwenzake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad