Tazama Picha za ziara ya Rais Kikwete mkoani Kagera akizindua Mradi mkubwa wa Maji, Mradi wa umeme Vijijini, Barabara, wilaya mpya ya Kyerwa na Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Ruvubu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 28, 2013

Tazama Picha za ziara ya Rais Kikwete mkoani Kagera akizindua Mradi mkubwa wa Maji, Mradi wa umeme Vijijini, Barabara, wilaya mpya ya Kyerwa na Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Ruvubu.

Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani Biharamulo mkoani Kagera ambapo Katika hotuba yake ya utangulizi waziri wa ujenzi Dk John Magufuli amesema barabara hiyo kutoka
imejengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 191 ikiwa ni fedha zinazotolewa na serikali ya Tanzania ambapo mtendaji mkuu wa Tanroads injinia Patrick Mfugale amesema kazi hiyo ambayo imeshakamilika kwa asilimia 96 inatarajiwa kukamilika mwezi ujao.

Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na Wananchi wa Rusumowilayani Ngara Mkoani Kagera  baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Ruvubu ambapo akiwahutubia Wananchi wilayani  humo alisisitiza suala la  kuanza operesheni kali ya kuwasaka majambazi wanaojihusisha na uhalifu ikiwemo utekaji wa magari na wahamiaji haramu itayoanza wiki mbili zijazo na ameagiza wahusika kuanza kujisalimisha wao na silaha wanazomiliki kinyume na utaratibu.  

Ni Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika  kikiwa ndani ya Mto Ruvubu wilayani Ngara Mkoani Kagera , kilichozinduliwa na Rais Kikwete na  akawahimiza Wananchi wanaokitumia  kuhusu umuhimu wa kukitunza ili kidumu kwa miaka mingi.

Mara baada ya uzinduzi wa Kivuko hicho, Rais Kikwete amesema  kuwa mpango wa kujenga kituo cha kuzalisha nishati ya umeme wa maporomoko ya maji ya Rusumo wilayani Ngara umekamilika na kwamba utatumiwa na nchi tatu za Tanzania ,Rwanda na Burundi.


Rais Kikwete amesema kwa muda mrefu serikali imekuwa ikitafuta  fedha kwa ajili ya kuanza kwa mradi huo, na kwamba  kazi inayobaki ni ya kuanza kwa ujenzi huo ambao utakuwa na faida kwa Watanzania kwa kuongeza  uzalishaji wa nishati ya umeme kwa ajili ya kusambaza  katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
Ni muonekano wa Kivuko cha zamani  kilichokuwa kikitumiwa na Wananchi wa Ngara kuvuka mto Ruvubu.

Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu jana Jumamosi (Julai 27,2013).

Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasalimia katika Machimbo ya Busiri wilayani Biharamulo wakati akielekea wilayani Ngara pamoja na mkutano wa hadhara ,pia kuzindua kivuko cha Ruvuvu .

Rais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Ruvubu wilayani Ngara mkoani Kagera.

Rais Kikwete akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Rulenge,Wilayani Ngara wakati akiwasili kwenye kiwanja cha kijiji hicho tayari kwa kuzungumza nao ikiwa ni sehemu ya Ziara yake ya Kikazi Mkoani Kagera.

Rais Kikwete akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Rulenge,Wilayani Ngara wakati akiwasili kwenye kiwanja cha kijiji hicho tayari kwa kuzungumza nao ikiwa ni sehemu ya Ziara yake ya Kikazi Mkoani Kagera.

Hapa ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Prof Anna Tibaijuka akielezea baraza la ardhi baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi juu ya wilaya ya Ngara kupata Baraza la Ardhi ambalo litaendesha na kutatua migogoro ya ardhi.Kushono ni Rais Kikwete akisikiliza kwa Makini katika mkutano huo Kijijini Rulenge wilayani Ngara.

Ni muonekano wa Umati wa Watu ukimsikikliza Rais Kikwete  akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Rulenge,Wilayani Ngara mkoani Kagera.
Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa.

Rais Kikwete akiongea na wananchi katika sherehe ya kuzindua mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Nyaishozi, Wilaya ya Karagwe Rais Jakaya Kikwete alipokuwa mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku nane.

Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa wakati Rais Jakaya Kikwete  alipokuwa mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku sita.

Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa wakati Rais Jakaya Kikwete  alipokuwa mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku sita.

Rais Kikwete akikata utepe kuzindua mradi mkubwa wa maji  wilayani Muleba mkoani Kagera huku kushoto kwake akiwa ni Waziri wa Maji,Prof. Jumanne Maghembe na kulia kwake ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Prof Anna Tibaijuka.

Waziri wa Ardhi Profesa Anna Tibaijuka akishiriki katika ngoma ya utamaduni wakati wa mapokezi ya Rais Kikwete wilayani Muleba mkoani Kagera.

Vikundi vya ngoma vikitumbuiza wageni wakati  ziara yake ya siku sita Mkoani Kagera.

Wananchi wa Muleba wakimshangilia Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili wilayani humo akiwa katika ziara yake ya siku sita Mkoani Kagera.

Rais Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa Wananchi wa Muleba baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji kwa wilaya hiyo.

Vikundi vya ngoma vikitumbuiza wageni wakati  ziara yake ya siku sita Mkoani Kagera.

Rais Kikwete akijiunga na waumini wa wilaya ya Muleba kusali swala ya Magharibi kabla ya kufuturu wakati huu Waislam Duniani wakiwa katika Mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.


Dua ikisomwa baada ya futari aliyoandaa Rais Kikwete kwa wananchi wa Muleba.
Rais Kikwete akisalimia wananchi akiwa katika ziara yake ya siku sita Mkoani Kagera.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad