Wanasayansi
wa maabara ya Bristol Robotics Uingereza wamegundua njia ya kutumia mkojo kama
chanzo cha kuzalisha umeme wa kuchaji betri za simu, na kudai kuwa wa kwanza
kutengeneza “the world’s first microbial fuel cells (MFC) powered mobile
phone”.
Watafiti hao walielezea juu ya ugunduzi wao kupitia jarida la ‘Physical Chemistry Chemical Physics’.
Dr Ioannis
Ieropoulos amesema, huo ndio ugunduzi wa kwanza wa kuzalisha nguvu ya umeme kwa
kutumia mkojo, na katika majaribio ya utafiti huo wamefanikiwa kuchaji simu ya
Samsung.
Wanasayansi hao wanaamini kuwa teknolojia yao inaweza kutumika katika mabafu huko mbeleni kwaajili ya kuwashia mashine za kunyolea au kupasha moto maji ya kuoga na kuwasha taa.
No comments:
Post a Comment