Makamu wa Rais wa Tanzania Dk
Gharib Bilal akiongoza viongozi mbalimbali na maofisa wa jeshi la JWTZ, Jeshi
la Polisi na wengine mbalimbali kupokea miili hiyo hapo Jana(Julai 20,2013).
|
Baadhi ya askari wa JWTZ wakibeba miili ya
wanajeshi wenzao waliouwawa Darfur kuiingiza kwenye magari maalum kabla ya
kuondolewa katika uwanja wa jeshi.
|
Miili ya
wanajeshi saba wa Tanzania waliokuwa katika kazi za kutekeleza ulinzi wa amani
wa kimataifa katika mkoa wa Darfur nchini Sudan imewasili Jumamosi na
ndege maalumu ya Umoja wa Mataifa.
Wanajeshi hao waliuwawa mwezi Julai, kufuatia shambulizi la ghafla wakiwa nchini Sudan.
Kaimu mkurugenzi wa habari wa JWTZ, Meja Joseph Masanja anasema miili hiyo imewasili Jumamosi majira ya saa kumi kasorobo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J. K. Nyerere na imehifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo hadi Julai 22 ambapo itaagwa rasmi.
Miili ya
wanajeshi hao saba iliyowasili jana (Julai 20,2013) ni SajIni Shaibu Sheha Othman, Koplo Osward
Paulo Chaula, Koplo Mohamed Juma Ally, Koplo Mohamed Chukilizo, Private Rodney
Ndunguru, Private Peter Werema na Private Fortunatus Msofe.
Wanajeshi hao
walikuwa sehemu ya Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa (Unamid), kusini
mwa Darfur na walitoka katika vikosi vya, 42KJ Chabruma, Songea, 44KJ Mbeya,
36KJ Msangani, 92KJ Ngerengere, 94KJ cha Mwenge, Dar es Salaam, 41KJ Nachingwea
na Makao Makuu ya JWTZ- Upanga, Dar es Salaam.
Wakati taratibu
za maziko zikiandaliwa mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya
uhalifu wa kivita ICC Fatou Bensuda ametoa onyo kali kuhusu shambulizi la hivi
karibuni lililowalenga waangalizi wa amani kutoka umoja wa mataifa na jeshi la
umoja wa afrika huko Darfur sudan na kusema kuwa linaweza kuhesabika kama
uhalifu wa kivita.
Katika taarifa
yake akiwa Heague Fatou Bensuda amekumbusha pande zote zenye mgogoro kufahamu
kuwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ina mamlaka jimboni Darfur.
Rais Kikwete. |
Aidha RAIS
wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na
Rais wa Sudan Omar Bashir kufuatia kuuawa na kujeruhiwa kwa askari wa Tanzania,
walioko katika ulinzi wa kimataifa wa amani katika jimbo la Darfur na kumtaka
Rais Bashir kuchukua hatua za haraka kuwasaka na kuwakamata waliohusika na
kitendo hicho kiovu na kuwafikisha mbele ya sheria haraka
iwezekanavyo.
Katika mazungumzo
yao, Rais Omar Bashir amekubaliana na Rais Kikwete na kumuahidi kuwasaka hadi
kuwakamata wale wote waliohusika na kuwachukulia hatua za kisheria.
Rais Bashir amemueleza Rais Kikwete kuwa binafsi anaamini kuwa waliohusika ni wahalifu na hivyo kuahidi kuwa lazima watasakwa hadi kukamatwa kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.
Rais Bashir
amempa pole Rais Kikwete kwa tukio hilo la kusikitisha ambapo wanajeshi wa
Tanzania wameenda nchini Sudan kulinda Amani na Usalama wa wananchi wa Sudan.
Mapema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Bw. Ban Ki Moon alimpigia Rais Kikwete na kumpa pole kwa mkasa huo mkubwa na wa kusikitisha ambao umewatokea wa Tanzania hao wakati wakiwa katika kutekeleza jukumu lao la kulinda amani nchini Sudan.

Hadi sasa hakuna
kikundi chochote ambacho kimekiri kuhusika na shambulio hilo ingawaje kumekua
na kutupiana lawama baina ya vikundi vya kiserikali na vya waasi katika jimbo
la Darfur.
Mapigano baina ya
vikundi vya kikabila na koo mbalimbali zimesababisha mapigano na uvunjifu
mkubwa wa amani na usalama katika jimbo la Darfur kwa muda wa miaka 10 sasa, na
mara nyingi mapigano na tofauti zao hizo zimesababisha vifo na uvunjifu wa
amani kwa wananchi wa Sudan na wageni pia.
Mwishoni mwa mwaka jana Wanajeshi wanne kutoka Nigeria waliuawa karibu na El Geneina , Magharibi mwa Darfur ambapo pia inaelezwa na Umoja wa Mataifa kuwa wanajeshi wapatao 50 wameuawa tangu kikosi hiki cha Umoja wa Afrika kinachoundwa kwa pamoja chini ya Umoja wa Mataifa (UNAMID) kianze operesheni yake mwishoni mwa mwaka 2007.
Taarifa za Umoja wa Mataifa pia zinaeleza kuwa kabla ya mashambulizi yaliyofanyika dhidi ya kikosi cha Tanzania jumamosi iliyopita, wanajeshi 6 wanaolinda Amani wameuawa tangu oktoba mwaka Jana huu ambapo pia inasadikiwa kuwa watu wapatao 300,000 wameyakimbia makazi yao.
Hata hivyo kiini cha mgogoro huo unaosadikiwa kuwa ni ugomvi wa ardhi na rasilimali zilizoko katika jimbo hilo nchini Sudan.

No comments:
Post a Comment