Njiwa akiwa
amedhoofu kwa Baridi akiwa katika choo cha wanaume.
|
Njiwa akiwa
na ujumbe wa barua kama inavyo onekana.
|
Mashuhuda
wakitoka eneo la tukio.
|
Hii ni
sehemu alipokutwa Njiwa huyo.
|
Majengo nje
ya Ofisi ya Afisa Mwajiri.
|
Baadhi ya
wafanyakazi wakielekea eneo la tukio.
|
Afisa
Mwajiri (Mwenye shati ya bluu) Na baadhi ya wafanyakazi wakishuhudia tukio
hilo.
|
Juu na Chini ni Barua
iliyoletwa na Njiwa maeneo ya Ofisi ya Mwajiri upande wa mbele na nyuma.
|
Jengo la
Ofisi ya Afisa Mwajiri.
|
Stesheni ya
TAZARA kituo cha Mbeya.
|
ANGALIZO:
UNAPOTUMIA HABARI HIZI USIPOTOSHE UKWELI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0787-490 752
Au 0654-221465.
PICHA ZOTE
NA MBEYA YETU.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli, kati ya Tanzania na
Zambia(TAZARA) jana walijikuta katika wakati mgumu na baadhi yao kulazimika
kuzikimbia ofisi zao, baada ya ndege aina ya njiwa kukutuwa katika moja ya choo
cha ofisi hiyo akiwa amefungwa hirizi shingoni, huku akiwa na barua yenye
ujumbe wa onyo kali.
Tukio hilo
la aina yake, lilitokea mapema leo saa
mbili asubuhi katika ofisi za mamlaka hiyo zilizopo eneo la Iyunga Mkoani hapa,
hali ambayo mbali na baadhi ya wafanyakazi wake kuzikimbia ofisi, ilisababisha
kuibuka kwa mjadala mkubwa dhidi ya tukio hilo.
Mtandao huu
ulifanikiwa kushudia njiwa huyo mweusi akiwa nyuma ya choo cha kiume katika
eneo hilo la ofisi ya mwajiri, huku akiwa amefungwa hirizi shingoni
iliyozungushiwa shanga mchanganyiko wa rangi tatu, ambazo ni Nyekundu,
Njano na Nyeupe.
Mbali ya
kuwa na hirizi hiyo, pia njiwa huyo alikuwa amebeba barua inayodaiwa kuwa ni ya
mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo (jina limehifadhiwa kwa sababu maalumu)
ambaye anadaiwa hivi karibuni kufukuzwa kazi kwa makosa ya ubadhirifu.
Barua hiyo
ilikuwa na maandishi mekundu yenye ujumbe ulioandikwa kwa lugha mbili za
Kiswahili na kiarabu, ambapo katika maandishi ya Kiswahili yalisomeka “ Naomba
majibu haraka kama mtarudisha binti huyu kazini” ilisema sehemu ya ujumbe huo,
huku ikiwa na orodha ya majina matatu ya viongozi wa shirika hilo.
Mbali na
ujumbe huo ukiwa umeandikwa kwa maandishi ya mkono yaliyokolezwa kwa wino
mwekundu upande wa nyuma, lakini upande wa mbele kulikuwa na maandishi yakiwa
ni barua ya kutaarifiwa kufukuzwa kazi kwa mfanyakazi huyo.
Akizungumzia
tukio hilo, Mwajiri wa mamlaka hiyo kanda ya Mbeya, aliyejitambulisha kwa jina
la Mchaba Mgweno, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba waliobaini ni
wahudumu wa usafi.
Aliongeza
kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo aliwaarifu na wafanyakazi wenzake ambao
walikusanyika na kumshuhudia Njiwa huyo mweusi akiwa amedhoofika huku akiwa na
barua hiyo yenye vitisho.
Alisema
baada ya kushuhudia hali hiyo waliamua kutoa taarifa kituo cha polisi kilichopo
ndani ya shirika hilo, ambapo waliichukua barua hiyo na baadhi ya wafanyakazi
hao wakienda kutoa maelezo kituoni hapo.
“Kwa kweli
hali hii si ya kawaida, ila kwa sasa siwezizungumzia chochote kwa kuwa hata
mimi tukio hili limeniweka katika wakati mgumu na nimeshindwa kuendelea na
majukumu yangu ” alisema Mgweno.
Hata hivyo
kuliibuka malumbano makali kati ya wafanyakazi wa shirika hilo walioshuhudia
tukio hilo, ambapo baadhi yao wakidai kuwa tukio hilo ni la kutengenezwa kwa
lengo la kuchafuana.
“Hebu
angalia hiyo barua yenyewe mbona ni kivuli (Photocopy), kama ingekuwa ni ya
….wanamtaja mfanyakazi aliyefukuzwa jina limehifadhiwa ingekuwa ni nakala
halisi….haiwezekani mambo haya ni kutaka kuchafuana tu” alisema mmoja wa
wafanyakazi hao.
Lakini
baadhi yao wakiamini kweli kuwa barua hiyo ilitumwa ili itoe vitisho kwa
viongozi wa shirika hilo.
Baadhi ya
askari polisi wa kituo cha Tazara walikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba
wanaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli wake.
“Ndugu zangu
nyie mnajua taratibu za utoaji wa taarifa kwa jeshi hili, maana wapo wahusika,
lakini kwa kifupi sisi tulipokea taarifa na tunaendelea kuzifanyia kazi”
alisema mmoja wa askari hao.
Hata hivyo,
hadi tunapoondoka eneo la tukio majira ya saa sita mchana Njiwa huyo alikuwa
bado yupo eneo la tukio.
No comments:
Post a Comment