Tazama Picha za Misa ya shukrani ya Padre Ansigar Patrick Kaisile iliyofanyika katika Parokia ya Rinyana Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 22, 2013

Tazama Picha za Misa ya shukrani ya Padre Ansigar Patrick Kaisile iliyofanyika katika Parokia ya Rinyana Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara .


Kushoto ni Padre Johnbosco mhasibu wa jimbo la Rulenge-Ngara akiwa na Paroko wa Rwinyana Padre Patrick Kalile wakielekea kutabaruku makaburi katika misa ya shukrani ya Ansigar Patrick kaisile.


Kushoto ndiye Padre Kataisile akiwa na Mwenzake kutoka Songea.


Mapadre wa Parokia ya Rulenge na Rwinyana na waliotoka Peramiho songea wakisali kwa pamoja katika ibada ya shukrani kwa Padre Ansigar baada ya kupata daraja la upadre may 30 mwaka huu huko Songea.


Masister wa Nyabihanga parokia ya Rwinyana na waumini wa parokia hiyo wakiwa katika ibada ya kutabaruku makaburi ya familia ya padre Asigar Kaisile nyumbani kwao Kilinzi Rwinyana Ngara.


Mbunge wa Ngara akiwa na mwl Ghaitani Francis Nturo ( kaka yake padre Ansigar ) pamoja na masister wakiwa katika ibada ya kutabaruku makaburi baada ya misa ya shukrani.


Mwana blog yetu akisalimiana na Fr Ansigar nyumbani kwa wazazi wake eneo la kilinzi kijiji na parokia ya Rwinyana mara baada ya kukamilika kwa ibada ya misa ya shukrani kwa waliomuwezesha kupata daraja la upadre.(Picha na Shaaban Nasibu Ndyamukama)  


Vijana wa rika na madhehebu mbali mbali wametolewa rai ya kuwa  na uvumilivu katika harakati za kukabiliana na changamoto za maisha zikiwemo za miito mitakatifu mbele za Mungu.

 

Wito huo umetolewa jumapili ya wiki iliyopita na Padre Ansigar Patrick kaisile kutoka Peramiho ya songea mkoani Ruvuma wakati wa misa ya shukrani katika parokia ya Rinyana jimbo katoliki la Rulenge Ngara baada ya kupata daraja hilo miaka 38 iliyopita.



Padri kaisile akiongea na kipindi hiki muda mfupi mara baada ya sherehe za shukrani katika Parokia ya Rwinyana wilayani Ngara amesema kuwa vijana wengi wanashindwa kutimiza malengo yao kwa kukosa uvumilivu na kushindwa mitihani katika maisha yao.



Amesema kuwa vijana wajitokeze  katika miito ya kumtumikia mungu kwa kujiunga na mashirika ya kitume na kujifunza maadili ya kiroho na fani  mbalimbali zitakazowasaidia kulipa fadhira kwa wazazi na jamii wanakozaliwa au kutumikia katika kueneza neon la Mungu.



Aidha amewashukuru waliofanikisha yeye kupata daraja la upadre tangu aanze kuweka nadhiri tangu mwaka  1978 wakiwemo walimu wa dini shule ya msingi na sekondari pamoja na mashirika yaliyomuongezea ujuzi akiwa Afrika ya kusini kusomea utaalamu katika nishati ya umeme.



Kwa upande wake Padre Angelo Msele kutoka shirika la Mtakatifu Benedicto lililoko peramiho wilayani songea mkoani Ruvuma katika kuzungumza na kipindi hiki amesema wazazi wanalo jukumu la kupeleka watoto wao katika shule za elimu zenye mafunzo ya kiroho  kuwajengea nidhamu katika maisha yao.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad