Mkuu wa Mkoa wa kagera
Kanal Fabian Masawe.
|
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA
MITAA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 22 JULAI, 2013
HALI YA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MASHUJAA KITAIFA JULAI
25, 2013 NA ZIARA YA
MHESHIMIWA
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
MKOANI KAGERA.
Ndugu
Wananchi, kama ambavyo
nimewahi kuwajulisha mara nyingi kupitia vyombo vyetu vya habari juu ya Mkoa
wetu wa Kagera kupewa heshima kubwa ya kuandaa maadhimisho ya Siku ya
Kumbukumbu ya Mashujaa kitaifa mwaka 2013, leo napenda kuwajulisha juu ya
maandalizi ya maadhimisho hayo ambayo yataadhimishwa tarehe 25/07/2013 hapa
mkoani kwetu katika Wilaya ya Muleba katika Kambi ya Jeshi la Wananchi Kaboya.
Pia nawajulisha kuwa maadhimisho hayo yataambatana na ziara ya kikazi ya
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkoa wa Kagera.
MAADHIMISHO
YA MASHUJAA MWAKA 2013.
Ndugu
Wananchi, Maandalizi ya
maadhimisho ya Siku ya Kumbumbu ya Mashujaa mkoani Kagera yanaendelea vizuri
kamati mbalimbali za maandalizi zinatekeleza majukumu yake ya mwisho ili
kufanikisha maadhimisho siku ya Alhamisi ya wiki hii tarehe 25 Julai, 2013.
Kamati
zinazoandaa maadhimisho hayo ni Kamati ya Mapokezi, Usafiri na
Malazi; Kamati ya Ujenzi Uwanja na Mapambo; Kamati ya Chakula na Afya; Kamati
ya Ulinzi na Usalama; na Kamati ya Burudani, Habari na Uhamasishaji.
Ndugu
wananchi, Kwa kiwango
kikubwa maandalizi yote yamekamilika na tunatarajia kuanzia leo kupokea wageni
kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya mkoa, pia nje ya nchi watakaohudhuria
maadhimisho hayo.
Mkoa
wetu umejipanga vizuri kuwapokea wageni wote watakofika mkoani hapa kwa ukarimu
na bashasha kubwa.
Wajibu
wa Wananchi.
Ndugu
wananchi, Napenda
kutumia fursa hii kuwaomba kuwa wakarimu kwa wageni wetu wote
tunaowatarajia kuanzia leo kwa kutekeleza majukumu yenu kama
Wanakagera kama ifuatavyo;
Ø Kila mwananchi
kuhakikisha maeneo yake na mazingira yanayomzunguka yanaendelea kuwa katika
hali ya usafi kama utamaduni wetu. Pia kumwajibisha mtu yeyote atakaeonekana
anachafua mazingira yetu. Hili ni jukumu la kila mwananchi.
Ø Kila mwananchi
kushiriki kikamilifu katika kuadhimisha Siku yenyewe ya Kumbukumbu ya Mashujaa
tarehe 25 Julai, 2013 huko Kaboya Wilayani Muleba. Kwani
hatuna budi kuwakumbuka Mashujaa wetu kwa sababu ya historia ya mkoa wetu
kushiriki katika vita ya kumwondoa adui aliyekuwa amevamia nchi yetu kupitia
ardhi ya mkoa huu mwaka 1978 hadi 1979.
Ø Kila mwananchi
kuhakikisha anaitunza amani na utulivu kama destuli ya mkoa wetu kwa wakati
wote wageni wetu watakapokuwepo hapa mkoani na baada ya maadhimisho ya
Mashujaa. Aidha, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa imejipanga vizuri
kuhakikisha amani na utulivu vinatawala wakati wote.
Kwa mwananchi yeyote atakayeona viashiria vya uvunjifu wa
amani atoe taarifa mara moja ili taarifa hizo zifanyiwe kazi mara moja.
Wajibu
wa Vyombo vya Habari.
Ndugu
Wananchi, Vyombo vyetu
vya habari vina wajibu wa kuhakikisha vinaendelea kutoa taarifa mbalimbali kwa
wananchi kuhusu Maadhimisho ya Mashujaa kama ambavyo vimekuwa vikifanya kuanzia
mwezi Mei, 2013.
Aidha,
nawaombeni Waandishi, Wahariri na Wamiliki wa vyombo vya habari kutumia fursa
hii kuutangaza mkoa wetu wa Kagera katika sekta mbalimbali za uwekezaji na
fursa mbalimbali zinazopatikana katika mkoa wetu.
Vilevile
nawaombeni Wamiliki wa vyombo vya habari hasa redio zetu za jamii kutoa
muda wa kutosha katika vituo vyenu vya redio kurusha habari na matukio ya
Kumbukumbu za Mashujaa papo kwa papo (live coverage) siku ya maadhimisho
ili wananchi ambao hawatapata muda wa kufika Kaboya wazipate habari hizo kupitia
redio zetu za Jamii.
ZIARA
YA MHE. RAIS MKOANI KAGERA.
Ndugu
Wananchi, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye atakayekuwa mgeni Rasmi Katika
Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa tarehe 25 Julai, 2013. Pia Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika mkoa wetu wa
Kagera.
Ndugu
Wananchi, Katika ziara
hiyo Mheshimiwa Rais Kikwete anatarajia kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo
katika mkoa wetu kama ifuatavyo:
§ Kuweka
jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
§ Kuweka
jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ya Kagoma - Rusahunga .
§ Kuweka
jiwe la msingi barabara ya kiwango cha lami Kyaka hadi Bugene.
§ Kufungua
Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba.
§ Kufungua
jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd).
§ Kuzindua
mradi wa maji Muleba.
§ Kuzindua
kivuko kipya Rusumo (Ngara) .
§ Kuzindua
mradi wa usambazaji umeme vijijini Nyaishozi (Karagwe).
§ Kuzindua
Wilaya Mpya ya Kyerwa .
Ndugu
Wananchi, Vilevile
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataongea na wananchi kupitia
mikutano mbalimbali ya hadhara katika Wilaya zetu ndani ya mkoa.
Ndugu
Wananchi, nawaombeni
kujitokeza kuanzia tarehe 24/07/2013 uwanja wa ndege wa Bukoba ili kumpokea
Mheshimiwa Rais, pia atakapokuwa anafanya ziara katika Wilaya zetu tujitokeze
kwa wingi kumsikiliza.
Mwisho; Nawatakia ushiriki mzuri katika
kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa na mapokezi mazuri ya wageni wetu
hasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kagera:
Amani na Maendeleo.
Amani
na Maendeleo; Kagera.
Imetolewa na: Kanali Mstaafu
Fabian I. Massawe
Mkuu wa Mkoa
KAGERA
No comments:
Post a Comment