Baada
ya Maji kupungua katika eneo la Chipite ambalo lilijaa maji na kusababisha Abiria zaidi ya 500 na Magari
zaidi ya 200 kushindwa kupita eneo hilo
na Kufanya gari nyingi ziendazo na Kutoka Mtwara,Masasi,Ruangwa,Liwale,Nachingwea,Liwale,Nanyumbu
na Tunduru na kufanya safari kwa
kuzunguka wilaya ya Newala sasa hali imeanza
kubadilika na gari nyingi kuanzia jioni zimeanza kupita ingawa kwa Mashakamashaka ili kusaidia kupeleka na kutoa
huduma kwa Jamii.
Kufuatia
hali hiyo,Baadhi ya wasafiri waliokwama wametupia lawama kwa Wakala wa Barabara
Tanroads na Kitengo cha Maafa kutotoa Ushiriakiano wowote kuhakikisha Abiria wanakuwa salama
ikiwa pamoja na kutafuta jitihada za
haraka kuwavusha ili kuepusha Maafa yatakayochangiwa
na uwepo wa msongamano kwa muda mrefu.
Hali
ya usafiri sasa iko kama kawaida kuelekea katika wilaya Tajwa hapo Juu.
Picha na
Mdau Abdulaziz Lindi.
No comments:
Post a Comment