
Wabunge hao
walipanga kujilipa dola alfu mia moja na kumi kila mmoja kabla ya uchaguzi mkuu
ujao.
Lakini Bw.
Kibaki amesema kuwa hatua hiyo inakiuka katiba na haiwezi kutekelezwa wakati
ambapo walimu pamoja na madaktari nchini Kenya wamekuwa wakigoma kudai nyongeza
ya mishahara.
Waandamanaji
waliojawa na ghadhabu nchini Kenya walijitokeza hapo jana kulaani hatua ya
wabunge hao kutaka kujilipa mamilioni ya pesa kama pesa za ziada wakati bunge
litakapofunga vikao vyake kwa maandalizi ya uchaguzi mwaka ujao.
Waliwataja
wabunge hao kama fisi wenye ulafi.
Wabunge wa
Kenya ni baadhi ya wale wanaopokea mishahara mikubwa sana barani Afrika ,
wakipokea takriban dola elfu 10,000 kama mshahara kila mwezi.
Malipo hayo
ya ziada ya dola 110,000 kwa kila mmoja walitaka yalipwe wakati watakapofunga
vikao vyao kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2013.
Wadadisi
wanasema kuwa wananchi wangetozwa kodi zaidi ili kugharamia malipo hayo ya dola
milioni 23.
Hatua hii imewakasirisha
watu wengi, hasa ikizingatiwa kuwa inakuja baada tu ya migomo katika sekta ya
umma ambapo madaktari, walimu na hata wahadhiri wa vyuo vikuu walisusia kazi
wakidai nyongeza ya mishahara.
Mswaada huo
ulipitishwa siku ya Alhamisi ikiwa sehemu ya mabadiliko yaliyofanyiwa mswaada
wa fedha bungeni.
Mnamo mwezi
Septemba, shule za umma zilifungwa kwa wiki tatu wakati walimu walipogoma
wakidai nyongeza ya mishahara na huku madaktari nao wakitaka mazingira bora ya
kazi.
No comments:
Post a Comment