
Baadhi ya
Waandishi wa habari wa magezeti ya mbalimbali mkoani hapa wameshushwa katika
eneo la ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Manispaa ya Musoma na Afisa Mahusiano wa Mamlaka hiyo Emmanuel Ruyobya hali ambayo ni imeonekana kuwa ni
udhalilishaji.
“Kiukweli huu ni udhalilishaji kwani sisi tuna
vyombo vyetu ambavyo tunavifanyia kazi na si lazima tulipwe posho sasa huyu
yeye anasema bajeti finyu wakati sisi hatujaomba posho” alisema mmoja wa
waandishi wa habari walioshushwa katika gari hiyo.
Akisoma
taarifa ya Maendeleo na Changamoto zake
katika ofisi ya mkuu wa mkoa kwa Naibu,Katibu Tawala wa mkoa hupo Climent
Lujaji alimuagiza mkurugenzi wa MUWASA Genes Kaduri kuwaweza waandishi hao
katika suala la usafiri ili waweze kushiriki katika ziara hiyo ambapo
mkurugenzi huyo alimkubalia .
Aidha Baada
ya kuondoka katika eneo la ofisi wa mkoa waandishi wa habari hao walishishwa
katika gari hiyo kwa madai hayo na kwamba wameishaalika waandishi wao .
“Kama Katibu
Tawala wa mkoa ndiye kawaambia muje nendeni
awalipe na kuwatafutia usafiri.,alisema Afisa mahusiano Ruyobya kwa jaziba kubwa.
Tabia ya
kuwashusha waandishi wa habari si la
mara ya kwanza katika ziara mbalimbali zinazofanywa na viongozi kama hao mkoani
hapa hususani katika vyombo habari vya
magazeti kubaguliwa na hata hivi
karibuni 5 Oktoba mwaka huu imefanyika
ziara ya Naibu waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele ambapo pia vyombo vingine vimebaguliwa.
Naibu Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Binilith
Mahenge ameaza ziara yake ya kujua
maendeleo na changamoto zake mkoa wa
Mara ambapo imeanzia katika halmashauri
ya wilaya ya Manispaa ya Musoma,Butiama kukagua
chanzo cha maji cha Mugango –Kiabakari, Rorya,Serengeti na kumalizia
wilaya ya Bunda.
No comments:
Post a Comment