Katika kuadhimisha Simba Day ,klabu hiyo yatembelea Wagonjwa na kugawa zawadi mbalimbali. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 08, 2012

Katika kuadhimisha Simba Day ,klabu hiyo yatembelea Wagonjwa na kugawa zawadi mbalimbali.

Kaburu (kulia) akitoa mawili matatu wakati Simba ilipotembelea wagonjwa na kutoa zawadi leo huku ,  Lengo letu ni kusaidia jamii hivi kila mara.


Viongozi, wachezaji na wazee mbalimbali wa mabingwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba wamefanya tukio la kihistoria leo baada ya kutembelea wagonjwa kwenye Hospitali ya Mwanaymala jijini Dar es Salaam na kugawa misaada mbalimbali.

 

 

Tukio hilo nadra kuonekana likifanywa na klabu za soka nchini limeelezewa na uongozi wa Simba kuwa ni sehemu ya wiki ya maadhimisho ya siku maalum ya kila mwaka ya klabu hiyo ya 'Simba Day'.


Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Nyange 'Kaburu' ndiye aliyeongoza msafara huo huku kwa upande wa wachezaji, kipa na nahodha Juma Kaseja ni miongoni mwa nyota walioshiriki kukabidhi misaada hiyo, akiambatana na nyota wenzake kadhaa wakiwamo Juma Said Nyosso, Kigi Makassy na kiungo aliyesajiliwa msimu huu kutoka Kenya, Salim Kinje.

 

Sisi ni watu wa kujali jamii bwana... Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange 'Kaburu' (katikati) akiwa pamoja na nahodha wa timu hiyo, Juma Kaseja (kulia) na beki Juma Nyosso (kushoto) wakibeba vyandarua na zawadi nyingine kwa ajili ya kugawa kwa wagonjwa wakati walipotembelea hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.


Afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga akijiandaa kumwaga vyandarua hospitalini Mwananyamala leo.


Akizungumza hospitalini hapo, Kaburu alisema kuwa wamewatembelea wagonjwa na kuwapa misaada kwa vile klabu yao ni sehemu ya jamii na hivyo wanapaswa kurejesha kidogo wanachokipata kwa kuwajali watu wenye mahitaji maalum.

 

Akaongeza kuwa mbali na kutembelea wagonjwa, pia watatembelea baadhi ya vituo vya watoto yatima na kuwapelekea misaada mbalimbali.


Baadaye, msafara huo wa Simba uliowatembelea wagonjwa waliolazwa katika wodi ya akina mama wajawazito na pia ya watoto waligawa vitu mbalimbali kama vyandarua, maji na sabuni.


Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Sophinias Ngonyani, aliwashukuru viongozi na wachezaji wa Simba kwa hatua yao ya kuwatembelea na kugawa misaada kwa wagonjwa; huku pia akiziasa klabu za soka na wanamichezo wengine kuiga moyo huo.

 

Leo sio mwisho, tutakuja tena na tena... Kaburu akizungumza na akina mama hospitalini Mwananyamala.


Katika tukio mojawapo la kusisimua hospitalini hapo, mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Rose Joseph alisema kuwa amefurahi sana  kuwaona 'live' wachezaji wa timu anayoishabikia ya Simba an kwamba, ameamua kumpa jina la 'Juma Kaseja' mtoto wake aliyemzaa leo asubuhi kwa vile alipata bahati ya kubebwa na kipa huyo nyota wa 'Wekundu wa Msimbazi' na timu ya taifa, Taifa Stars.


“Nimefurahi sana kumuona Kaseja akimbeba mwanangu,” alisema Rose.

 

Hii ndio Coaster yetu lakini basi kubwa la kisasa linakuja Agosti 15.

 Source:http://straikamkali.blogspot.com

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad