Wakati Mkutano wa nane wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania unatarajia kuanza leo mjini Dodoma ,Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutumia Billioni 648 Bajeti ya 2012-2013. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 12, 2012

Wakati Mkutano wa nane wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania unatarajia kuanza leo mjini Dodoma ,Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutumia Billioni 648 Bajeti ya 2012-2013.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Zanzibar anayeshughulikia Fedha Uchumi Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee (pichani) akiwasilisha mwelekeo wa Bajeti ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 ambapo makadirio ya mapato na matumizi ni Sh.bilioni 648.9.


Mkutano wa nane wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania unatarajia kuanza leo  mjini Dodoma ambapo miongoni mwa shuguli zitakazofanyika katika siku ya kwanza ni kuapishwa kwa wabunge wapya walioteuliwa.

 

Aidha Bajeti ya serikali inatarajiwa kusomwa siku ya alhamisi ijayo mjini domama bajeti ambayo itasomwa pia kwa wakati mmoja kwa nchi wanachama wa jumuiya ya Africa mashariki ambazo ni Kenya ,Uganda,Rwanda na Burundi.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Zanzibar anayeshughulikia Fedha, Uchumi , Mipango na Maendeleo, Omar Yussuf Mzee (kulia) akitoa taarifa ya mwelekeo wa Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 2012/2013 kwa wandishi wa habari kwenye ukumbi wa ofisi yake Vuga mjini Zanzibar .

Wakati huo huo kikao cha mkutano wa nane cha baraza la wawakilishi Zanzibar kinatarajia kuanza kesho kutwa ambapo pamoja na mambo mengine kikao hicho kitapitisha bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar katibu wa baraza la wawakilishi Yahya hamis Hamad amesema kikao hicho pia kitatoa taarifa kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi kuhusu sheria ya mabadiriko ya katiba mpya ya Tanzania .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad