Madereva wa magari madogo ya abiria mjini Ngara,mwishoni mwa wiki iliyopita waligoma kutoa huduma hiyo kwa zaidi ya masaa sita,baada ya dereva mwenzao kupigwa na askari polisi na kupelekea kulazwa katika hospitali ya Nyamiaga wilayani humo.
Katibu wa Chama cha madereva wa abiria wilayani Ngara Bw.Jacob Kilula, alimmtaja dereva aliyepigwa kuwa ni Ndayi Jacksoni,ambae alipigwa na askari polisi akimtuhumu kubeba abiria kupita kiasi.
![]() |
Hilo ndilo jeraha alilojeruhiwa Dereva Ndayi Jacksoni na Askari Polisi |
Nao baadhi ya madereva walioongea na Radio Kwizera,wamesema kuwa vitendo vya asikari wa jeshi la polisi kuwanyanyasa madereva hao vimeshamiri wilayani humo,hali ambayo hupelekea madereva hao kutofanya kazi zao kwa amani.
![]() |
Dereva Ndayi Jacksoni akiwa kalazwa katika kitanda cha wagonjwa katika Hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara akisubili kupatiwa huduma ya matibabu. |
No comments:
Post a Comment