Mashindano ya umoja wa michezo na taaluma shule za msingi Tanzania UMITASHUMTA yaanza kutimua vumbi lake Wilayani Ngara mkoani Kagera' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, June 13, 2012

Mashindano ya umoja wa michezo na taaluma shule za msingi Tanzania UMITASHUMTA yaanza kutimua vumbi lake Wilayani Ngara mkoani Kagera'

Kikosi cha soka cha timu ya UMITASHUMTA  Kata ya Ngara mjini kikijiandaa na mazoezi uwanja wa kokoto.

Mashindano ya umoja wa michezo na taaluma shule za msingi Tanzania UMITASHUMTA kwa michezo ya mpira wa miguu Wavulana na Wasichana,Mpira wa Netiboli Wasichana ,Mpira wa Wavu Wavulana na Wasichana ,Mbio mita 100,200,400,800,1500 na 3000 Wasichana na Wavulana,Mitupo pamoja na Miruko.

 

Mazoezi yakipamba moto chini ya kocha Mwl.Adof  Gisuka. 

Mashindano mengine yanayochezwa ni Taaluma  katika masomo ya Hisabati ,Insha,Kiingereza na Uchoraji.


Baadhi ya Wanafunzi kutoka shule za kata ya Ngara mjini wakifuatilia michezo mbalimbali ya UMITASHUMTA ya kata hiyo katika uwanja wa Kokoto. 

Mwl.Adof  Gisuka na baadhi ya Walimu wengine wa michezo wakitoa somo la michezo mbalimbali kwa wanafunzi kabla ya kuanza mashindano . 

Baada ya michezo mbalimba  ndipo Sospiter Mtegoa ambaye ni mratibu elimu kata,Mamlaka ya mji mdogo Ngara akatangaza wachezaji waliochaguliwa kuunda timu ya UMITASHUMTA  kwa kata hiyo.

 

Mita 100 -Wavulana  =  Juma Milele na Akupendae Henry huku Wasichana ni Sophia Julius na Debora Dauson.

 

Mita 200 – Wavulana  = Joasi Samson na Edward Masumbuka huku Wasichana  ni  Aleti Gidion na Saum  Mohamed.

 

Mita 400 – Wavulana  = Atupendae Henry na Nyabenda John  ili hali Wasichana ni pamoja na Jackline Didas na Nasmu Mohamed.

 

Mita 800 – Wavulana   = Juma Milele na Joasi Samsoni ili hali Wasichana Martha Edwin na Martha Brown.

 

Mita 1500 – Wavulana  =  Turuki Yasini  , Eric Philimon, Owen William(Mlemavu asiyesikia) na Majaliwa Tuombe  huku Wasichana ni  Janeth Mgisha ,Jackline Didas na  Saum Mohamed .

 

Mita 3000 – Wavulana   = Uchaguzi George,Stephano Sipirian na Baraka Ludovick huku Wasichana ni  Prisca Joseph ,Rose Jonathan na  Sara Savery.

 

Miruko – ni pamoja na Wavulana   = Alpha Salum , Eliyasa Yunus  na  Akupendae Henry  huku Wasichana  Aneth Gidion,Judith Kakwiti na Ester Eliakim.

  

 Netboll. 



Bijoy Josias, Christina Edward , Halima Twalib , Mawingu Abdallah , Neema Mfinanga , Lilian Leonard , Seprina Danford , Jenny Oscar , Felista Salvatory  na Vestina Shadrack.

 

  Mpira wa Miguu.


 

Makipa : ni Erisa Yunus na Jonathan Paschal.

 

Mabeki : ni pamoja na Akupendae , Joasi Samson, Wilfred Joansen , Paschal Kepha , Jackson Josephat  na Eric Philimon.

 

Viungo : ni  Kalama Steven , Donald Festo , Joel Joseph na Fidel Masenga.

 

Washambuliaji : ni pamoja na  Juma  Milele , Michael Mondest  na Alen Oscar.

 

Michuano hii ya UMITASHUMTA inafanyika ikiwa na changamoto nyingi katika vifaa vya kuchezea wanafunzi husika ,mfano ukosefu wa tufe,kisahani na vifaa vingine vya michezo kwa baadhi ya shule na wilaya hapa nchini.

 

Wachezaji hao waliochaguliwa watakuja kupambana   na kata zingine siku ya Alhamisi na ijumaa Juni 14 hadi 15 mwaka huu ili kuunda timu ya tarafa ya Nyamiaga ambayo itapambana na tarafa zingine  kuanzia Juni 18 hadi 19 mwaka huu  ili kuunda timu ya UMITASHUMTA wilaya ya Ngara.

 

Aidha walimu wa michezo wanaosimamia Mashindano hayo ya UMITASHUMTA wilaya ya Ngara mkoani Kagera wameiomba serikali  kuepuka zima moto  katika michuano hiyo kwa kufanya maandalizi ya kutosha ili kuleta ufanisi  katika michuano hiyo kwa shule za msingi.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad