Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Constantine Kanyasu awataka wakazi wa wilaya hiyo kuvipa nafasi vyombo vya sheria ili viweze kushughulikia tuhuma zinazowakabili baadhi ya askari polisi'' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, June 13, 2012

Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Constantine Kanyasu awataka wakazi wa wilaya hiyo kuvipa nafasi vyombo vya sheria ili viweze kushughulikia tuhuma zinazowakabili baadhi ya askari polisi''

Serikali wilayani Ngara imewataka wakazi wa wilaya hiyo kuvipa nafasi vyombo vya sheria ili viweze kushughulikia tuhuma zinazowakabili baadhi ya askari polisi wanaotuhumiwa kumushambulia dereva wa gari ndogo la abiria kwa kile kinachodaiwa kwamba alizidisha abiria .  


Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Constantine Kanyasu amesema kitendo kilichofanywa na asakari hao hakiwezi kuvumilika na lazima sharia ichukue mkondo wake.


Amesema askari hao wanashilikiwa na jeshi la polisi wakisubuliwa kufikishwa katika mahakama ya kijeshi kwa mujibu wa sheria za watumishi wa vyombo vya usalama kabla ya kufishwa katika mahakama za kiraia.

Bw Kanyasu amesema walishindwa kuchukua hatua haraka kutokana dereva huyo Ndayi Jackison alikuwa bado anapatiwa matibabu ambapo sasa ameshaandika maelezo yake kabla ya kufika mahakamani kutoa ushahidi wake juu ya tukio hilo  . 

Source:RK FM                                 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad