 |
Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa akisoma bajeti ya Serikali ya
2012/13, Bungeni Mjini Dodoma Juni 14, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
|
Waziri wa fedha na uchumi Dk William Mgimwa
leo amewasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ambayo nin sh
Trilioni 15 tofauti na ile ya mwaka unaomalizika ya Sh Trilioni 13.5,katika mwaka ujao wa fedha ambao huanza Mwezi July ya kila mwaka.
Bajeti hiyo ina vipaumbele 7 ambavyo ni Miundombinu, kilimo, viwanda,
rasilimali watu, huduma za jamii, utalii, pamoja na biashara ya ndani na nje na
huduma za fedha.
 |
Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa akionyesha mkoba wenye Bajeti
ya Serikali ya 2012/13 Bungeni Mjini Dodoma Juni 14, 2012. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
|
Bajeti hiyo imeelezwa kuwa itakuwa mwiba kwa mtanzania ambapo baadhi ya
bei za bidhaa (vinywaji na vileo )zimeongezwa kodi hali ambayo
ilisababisha migumo miongoni mwa wabunge na baadaye kutoa maoni yao.
Aidha waziri huyo ametangaza kuanza kwa mafunzo yay a lazima ya JKT kwa mwaka
huu ambapo jumla ya vijana 5000 wataanza mafunzo hayo pamoja na kutangaza kuajiri zaidi ya wataumishi elfu 70 katika sekta
mbalimbali.
 |
Mabalozi wa Nchi mbalimbali waliohudhuria Bungeni kusikiliza
Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2012/13 iliyosomwa na Waziri wa Fedha Dkt.
William Mgimwa, Bungeni Mjini Dodoma Juni
14,2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
|
Bajeti imelenga kuviwezesha viwanda vya ndani kuhimili soko la ushindani
kwa bidhaa zake dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.
Hali kadharika Bajeti hiyo imetoa
pendekezo la kulinda kazi za wasanii kwa kusajili kazi hizo ili kuwaingizia
faida ya kipato kitakacho wawezesha kunufaika na kazi zao.
Jeh! bajeti hii inayosomwa leo inakugusa kiasi gani Mtanzania
mwenzangu?
WAKATI HUO HUO BAJETI
YA SMZ YAWASILISHWA LEO MJINI ZANIZBAR BAJETI YA SMZ YAWASILISHWA LEO MJINI
ZANIZBAR .
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetangaza Bajeti
yake kwa mwaka 2012/13 ambayo pamoja na mambo mengine, imeongeza kodi katika
maeneo manane ikiwamo mafuta, ada ya bandari na ushuru wa stempu huku ikiwa na
maeneo sita ya kipaumbele.
Maeneo hayo ya vipaumbele ni afya, ajira kwa vijana,
ustawi wa wazee, elimu, kuimarisha uchumi na kuhifadhi mazingira ili
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
 |
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais anaeshughulikia Fedha na
Uchumi na
Mipango ya Maendeleo Zanzibar,Omar Yussuf Mzee akionesha
mkoba wenye nyaraka za Bajeti ya
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha
2012/2013 leo Nje
ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi(Picha na Yussuf
Simai,MAELEZO
Zanzibar)
|
SMZ katika
bajeti yake hiyo, imepanga kutumia Sh307.8 bilioni kwa kazi za kawaida na Sh341.1bilioni
kwa ajili ya shughuli za maendeleo huku makusanyo yakitarajiwa kuwa 648.9
bilioni.
Akiwasilisha Bajeti hiyo jana kwenye Baraza la Wawakilishi, Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais (Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo), Omar Yussuf Mzee alisema
kwa kuzingatia dhamira ya Serikali katika kukuza mpango wa maendeleo,
imependekeza marekebisho ya viwango vya tozo ya kodi.
 |
Waziri
wa Nchi Afisi ya Rais anaeshughulikia Fedha na Uchumi na
Mipango ya Maendeleo Zanzibar,Omar Yussuf Mzee akisoma bajeti ya SMZ
leokatika Baraza la Wawakilishi.(Picha na Yussuf Simai,MAELEZO
Zanzibar)
|
Mzee alitaja
mabadiliko hayo kwamba yamegusa Sheria ya Ushuru wa Stempu namba 6 ya
mwaka 1996, Sheria ya Kodi za Hoteli namba 1 ya mwaka 1995, Sheria ya Ada za
Bandari namba 2 ya mwaka 1999 na Sheria ya Ushuru wa Petroli namba 7 ya mwaka
2001.
Sheria nyingine ni ile ya Usimamizi na Utaratibu wa kodi namba 7 ya mwaka 2009,
Sheria ya kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) namba 4 ya mwaka 1998, Sheria ya
Bodi ya Mapato Zanzibar namba 7 ya mwaka 1996 na Sheria ya Mafunzo ya Amali
namba 8, ya mwaka 2006.
.
No comments:
Post a Comment