 |
Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka nje ya
viwanja vya Bunge la Tanzania jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli
ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge
huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13
katika mkutano unaoendelea. Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dodoma
|
MNYIKA
ANGEKUWA DHAIFU ZAIDI KAMA ANGEFUTA KAULI YAKE BUNGENI.
1. Kama udhaifu ni kuto kujua kwa nini wananchi wako ni maskini
wakati wako nchi tajiri. Mnyika yuko sahihi.
2. Kama huwezi kumuwajibisha au kuona madudu ya katibu mkuu au katibu
kiongozi mpaka bunge lishikilie bango na kushinikiza wang'oke ndio
uzinduke kufanya maamuzi basi mnyika yuko sahihi.
3. Kama kweli watu wamelibia taifa kupitia dili za magumashi halafu
una watangazia warejeshe fedha ili wasichukuliwe hatua na wakati
huohuo vibaka wanauwawa au kuchomwa moto kwa kuiba kuku na simu basi
ni dhahiri kuna udhaifu wa kiungozi. Mnyika yuko sahihi.
4. Kama ndege inaingia kwenye anga ya nchi yako na kubeba wanyama
kupeleka Arabuni bila hatua zozote kuchukuliwa ni dhahiri kuna udhaifu
wa kimfumo ulio kubuhu serikalini. Mnyika yuko sahihi.
5. Kama rais anafunga safari kwenda kuomba misaada na wakati huohuo
misaada anayopewa hailingani thamani na raslimali zinazo vunwa kwenye
nchi yake basi Mnyika yuko sahihi.
6. Kama rais anadiriki kutoa ahadi 99 ambazo thamani yake ni zaidi ya
trilion 9 huku akijua kuwa hazitekelezeki ni hadaa kwa wananchi, chama
na serikali. Mnyika yuko sahihi.
7. Kama taasisi ya Ikulu na mfumo wake wa utawala umehusika kuingilia
maamuzi ya mhimili wa haki kwa kutoa hukumu ya upendeleo ili kumkomoa
au kumnyang'anya mbunge wadhifa kama jinsi ilivyo lalamikiwa. Mnyika
yuko sahihi.
8. Kama serikali inatenga 70% kwa matumizi kwenye bajeti yake na 30%
kwenye maendeleo. Ni dhahiri kuwa ni aina ya serikali dhaifu yenye
viongozi wavivu wa kufikiri.
Kama hivyo ndivyo, nasimama na kijana mwenzangu kwa ukakamavu na
kupaza sauti yenye mwale mkali. Namuunga mkono Mnyika.
Mnyika amekisema kile kinachosemwa na baadhi ya wananchi wenye
ujasiri, tofauti yake na yetu ni kwamba yeye kasemea bungeni sisi
tunasemea vijiweni tukinywa kahawa.
 |
Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika akiteta na Mbunge
wa jimbo la Wawi Hamad Rashid Mohamed (kushoto) na Mbunge wa Bariadi Mashariki
John Cheyo mara baada ya kuondolewa Bungeni mjini Dodoma baada ya kukataa
kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa
dhaifu.
|
Aidha Mbunge
huyo wa jimbo la Ubungo Bw John Mnyika
katika Tamko lake baada ya kutolewa nje
ya Bunge kwa kukataa kufuta kauli yake kuwa Rais Kikwete ni DHAIFU ameendelea
kusisitiza kuwa ubovu wa bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2012/2013 ni matokeo ya udhaifu wa Rais Jakaya Kikwete kwani ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka
mitano.
Amesema
bajeti ya sasa haikuzingatia mpango wa Taifa ingawa imepita kwenye baraza la
mawaziri na kwamba kushindwa kutekelezwa
kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
Amesema Rais Kikwete anapaswa kumuagiza Waziri
wa Fedha kuiondoa bajeti na irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho.
 |
Mbunge
wa Ubungo (Chadema), John Mnyika akiingizwa na askari wa bunge kwenye gari
baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuamuru atolewe nje ya viwanja vya bunge baada
yambunge huyo kugoma kufuta kauli yake kuwa Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu,
wakati akichangia hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/13,
mjini Dodoma
|
Kauli hiyo
ya Mnyika inaonekana kutaka kujibu mapigo ya kikao cha juzi ambapo mbunge wa
Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba wakati akichangia bajeti, alisema kuwa
wapinzani ni wanafiki, waongo, wana mapepo na wanapaswa kuombewa na kupimwa
akili huku pia Mchango wa Lusinde ambaye ni Mbunge wa Mtera-CCM, akisema bajeti
ya upinzai ya uongo na haitekelezeki kwani yaliyoandikwa hayana uhusiano na
ilani ya uchaguzi wa Chadema, kwani waliwahi kusema watatoa elimu bure lakini
suala hilo halimo kwenye bajeti.
No comments:
Post a Comment