![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Fabian Massawe akiwahutubia
wanakamati wa kikao cha maendeleo mkoani kageraa.Mh. Massawe amesema wananchi
wanakiu ya maendeleo sio siasa.
|
Mkoa kagera unatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 196 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, misharara pamoja na matumizi ya kawaida katika kipindi cha mwaka 2012 /2013.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanal mstaafu Fabian Masawe amefafanua kuwa kiasi cha shilingi bilioni 128 zimeombwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na zilizobaki zimeombwa kwa ajili ya mishahara.
Kanal Masawe amesema kuwa fedha nyingine zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, matumizi mengineyo na kwamba bajeti hiyo imeongezeka kwa asilimia 5.9 ukilinganisha na bajeti ya mwaka wa fedha wa 2011 / 2012.
Mji wa Kamachumu- Muleba. |
Hata hivyo amewaomba wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri kuhakikisha bajeti hiyo inasimamiwa na kuziba mianya ya matumizi mabaya ya fedha za serikali.
Picha ikionyesha Migomba yenye Ugonjwa wa Mnyauko huku Baadhi ya wakulima wamekata tamaa na mashamba yao. |
No comments:
Post a Comment