NDEGE YA ATC ILIVYOPATA AJALI MKOANI KIGOMA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 12, 2012

NDEGE YA ATC ILIVYOPATA AJALI MKOANI KIGOMA.

Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC), aina ya Dash 8-300 iliyokuwa inatoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kupitia Tabora, ikiwa imeanguka jana baada ya kuteleza kutokana na tope jingi kuwepo kwenye njia ya kurukia ya Uwanja wa Ndege wa Kigoma. Abiria 35 na wafanyakazi wanne walinusurika kwenye ajali hiyo.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Kihenya Kihenya  amesema ndege aina dash  8 Q 300 yenye namba t.c 119 ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) iliyokuwa na abiria 35 pamoja wafanyakazi 4 ikifanya safari zake kutokea Kigoma kuelekea jijini Dar es Salaam imeanguka leo majira ya Saa 4 na dakika 15 asubuhi.
Amesema chanzo cha ajari ni matope kuwa kwenye bara bara iliyo pelekea ndege hiyo kushindwa kuruka na kupoteza uelekeo na kuvunja bawa la kulia.

Kamanda kihenya amesema hakuna madhara kwa abiria uchunguzi zaidi juu ya ajali hiyo unaendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad