Habari hii na BBC Swahili
Msanii wa kike wa filamu Tanzania Elizabeth Michael Kimemeta maarufu kama Lulu,amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwingine wa filamu Marehemu Steven Kanumba.
Amefikishwa mahakamani ikiwa ni siku nne, tangu alipokamatwa mara baada ya kifo cha msanii huyo ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi.

Mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam,Bi Augustina Mbando,Elizabeth Michael Kimemeta ajulikanaye kama Lulu kwa jina la Usanii,aliwasili mahakamani hapo akiwa chini ya Ulinzi mkali wa askari Polisi waliokuwa wamevaa kiraia na wengine wakiwa wamejihami kwa silaha.
Mara baada ya Kufikishwa mahakamani,upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa serikali Bi Elizabeth Kaganda ulimsomea shtaka moja ambalo ni la mauaji, kosa ambalo ni kinyume cha sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha 196.
Wakili huyo wa serikali Bi Elizabeth Kaganda,alidai mbele ya mahakama kuwa mnamo tarehe 07 mwezi April mwaka 2012,katika eneo la Sinza Vatican,msanii Elizabeth alimuua msanii Steven Kanumba.
Akiwa amevalia gauni kubwa lijulikanalo kama dera lenye rangi ya Njano mtandio wa rangi ya waridi na kandambili nyekundu mshtakiwa alionekana kutokuwa na wasi wasi pamoja uzito wa tuhuma za mauaji anayokabiliwa nayo huku akijibu maswali kadhaa kuhusu wasifu wake.
Msanii huyo alikanusha kuwa na umri wa miaka 18 baada ya kuulizwa ,ambapo yeye amesisitiza kuwa ana umri wa miaka 17, hii ikiwa ni tofauti na habari ambazo zimekuwa zikiripotiwa kuhusu umri wa msanii huyo ambaye sasa anatambulika kama mshtakiwa.
Kesi hii ya mauaji inatajwa kwa mara ya kwanza na mshtakiwa hakutakiwa kukiri wala kukana mashtaka.
Upande wa mashtaka umeieleza mahakama kuwa kesi bado iko kwenye upelelezi ambapo inatarajiwa kutajwa tena April 23 mwaka huu.
Mshtakiwa amepelekwa rumande hadi siku hiyo wakati kesi hii itakapotajwa tena.
Kwa upande mwingine tukio la kufikishwa mahakamani kwa mtuhumiwa huyo kumefanywa kwa usiri mkubwa na kufanya waandishi wa habari wengi wameshindwa kufuatilia kwa karibu tukio lenyewe.
Kufikishwa mahakamani kwa msanii huyo na kusomewa shtaka la mauaji ya Kanumba kumetokea siku moja baada na Marehemu Steven Kanumba kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni.
Mazishi yake yalichukua sura ya kitaifa kutokana na umaarufu aliojijengea msani huyo katika jamii ya watanzania na hata nchi za nje.
TUMEJIFUNZA NINI KATIKA MSIBA WA KANUMBA SISI VIJANA?
*.Hakuwa mbinafsi kwani tumeshuhudia vijana wengi kawaibua katika Filamu zake mbalimbali
*.Hakuwa na Majivuno Kwa kiwango alichokuwa amefika Kanumba leo angetafuta watu fulani wa kuongea nao lakini hakuwa hivyo
*.Alipenda jamii ndiyo maana aliweza kutoa misaada mbalimbali kwa makundi tofauti na ndiyo maana Jamii imejitokeza katika kumuaga

*.Hakukatishwa na Maneno ya watu wasiopenda mafanikio ya wenzao
*.Aliipenda sana nchi yake kwa dhati na popote alipenda kusema natoka Tanzania
*.Kanumba hakubagua huyu wala yule ndiyo maana kazikwa na watu wengi wa rika tofauti
*.Alikuwa kiongozi kwa wenzake.
*.Alichukia umaskini.
*.Kanumba alijipenda na alipenda kutengeneza Historia hapa Duniani
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo niliyajua kwa Kanumba baada ya kuwa na Mafanikio ya haraka katika tasnia ya Filamu,nilitamani sana kufika katika mazishi lakini sikuweza,aaaaah Kanumba ipo siku nitafika kwenye kaburi lako japo niseme neno ambalo siku zote nilipenda nikwambie lakini sikuweza kukutana nawe na hilo neno ni hili hapa HONGERA KAKA KWA KAZI ZAKO hili neno sijakwambia lakini ipo siku nitakwambia tutakapokutana katika uzima wa Milele

No comments:
Post a Comment