Chadema wametangaza kukata Rufaa Mahakama Kuu ya Rufaa Tanzania na kwamba Rufaa hiyo wanataraji kuikata hivi karibuni katika Mahakama kuu ya Rufaa Tanzania.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho Freeman Mbowe alisema zipo sababu tatu zilizowafanya waende kukata Rufani badala ya kuingia kwenye uchaguzi mdogo moja kwa moja.
Wakihutubia umati mkubwa wa wakazi wa Arusha na viunga vyake waliofruka katika viwanja vya NMC, mapema leo viongozi hao akiwepo Godbless Lema mwenye aliwasihi wananchi kuendelea kuwa watulivu na kuondoa hofu na anaimani watashinda.
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilitoa hukumu hiyo na kutengeua Ubunge wa Godbless Lema baada ya kumkuta na hatia ya kutumia lugha ya udhalilishaji na maneno ya kashifa dhidi ya mgombea wa Balozi Dk. Batilda Buriani katika uchaguzi wa mwaka 2010 alipokuwa akigombea kwa tiketi ya CCM.
No comments:
Post a Comment