MATOKEO YA MECHI ZA CHAMPIONS LEAGUE MARCH 28 2012. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 29, 2012

MATOKEO YA MECHI ZA CHAMPIONS LEAGUE MARCH 28 2012.

Bayern Munich wametia mguu mmoja ndani ya Nusu fainali baada ya kupata ushindi wa ugenini dhidi ya Marseille wa bao 2-0 katika mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.


Bao za Bayern zilifungwa na Mario Gomez Dakika ya 44 na Arjen Robben katika Dakika ya 69.

Nao Mabingwa wa Ulaya, FC Barcelona, wameshindwa kuwika ndani ya San Siro walipotoka sare ya 0-0 na AC Milan kwenye mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Timu hizi zitarudiana huko Nou Camp  na  Allianz Arena hapo Aprili 3.

Marudiano

[Mechi ni Saa 3 Dak 45 Usiku]

Jumanne Aprili 3

Bayern Munich v Marseille

FC Barcelona v AC Milan

Jumatano Aprili 4

Real Madrid v APOEL Nicosia

Chelsea v Benfica

NUSU FAINALI

MECHI kuchezwa Aprili 17/18 na Aprili 24/25

Marseille/Bayern Munich v APOELNicosia/Real Madrid

Benfica/ Chelsea v AC Milan/FC Barcelona

FAINALI

MECHI Kuchezwa Mei 19 Allianz Arena, Munich

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad