Jaji wa mahakama kuu kanda ya Tabora Bi.Stella Mugasha amefuta kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Ubunge, iliyokua inamkabili mbunge wa jimbo la kigoma mjini Bw.Peter Serukamba, kutokana na upande wa madai kukaidi amri ya mahakama kwa kushindwa kupeleka mashahidi.
Mwanzoni mawakili wa upande wa mdai ambae ni Bw.Ally Mleh walijitoa katika kesi hiyo kwa kile walichodai kutoridhishwa na mwenendo wa kesi, na hivyo mlalamikaji kuomba apewe muda wa kutafuta mawakili wengine lakini alishindwa huku akipinga kesi hiyo kuendelea kusikilizwa na Jaji Mugasha.
Baada ya uamuzi huo kutangazwa, Bw.Serukamba amesema “nimefurahi sana kwa sababu haki imetendeka na imeonyesha mahakamani sio sehemu ya kupelekwa majungu, sio sehemu ya kupeleka maneno ya kwenye vijiwe vya kahawa kwa sababu ukiangalia kesi yenyewe ni kesi tu ya watu ilitengenezwa kutokana na kujaa chuki, lakini wao wenyewe wamekuja kushindwa kuiendesha kesi yao na mawakili wao wamejitoa”
Aidha Bw.Ally Mleh ambae ndo mdai, amesema “uamuzi uliotolewa na mahakama unamkatisha tamaa yeye na watanzania kwa sababu tulipokwenda mahakamani mwanzoni tulikua tunaamini kwamba Mahakama itatenda haki ya mdai na wadaiwa, kwa sasa hivi sina imani kabisa na kutokana na uamuzi uliotolewa na jaji huyu, kwa hiyo nitakata rufaa katika mahakama kuu ya rufaa na ina maana haki yangu itatendeka”
Katika hatua nyingine Mahakama kuu inayoendelea na vikao vyake vya kusikiliza maombi ya kupinga ushindi wa ubunge wa Mh. Tundu Lissu imeahirisha kikao chake baada ya wakili wa waleta maombi msomi Godfrey Wasonga kuugua malaria ghafla.
Kabla ya kuanza kwa kikao , wakili wa kujitegemea kutoka Dodoma mjini Wasonga, alisimama na kumwomba Jaji Mosses Mzuna, kuahirisha kikao hicho hadi afya yake itatengamaa na kuimarika.
Akifafanua wakili Wasonga alisema alipata homa ghafla iliyochangia asipate usingizi vizuri.
Kwa upande wake mlalamikiwa wa kwanza Mh. Tundu Lissu alitoa angalizo kwa mahakama hiyo kuu, kwamba upande wa waleta maombi wamekuwa wakiwasilishwa na mawakili wasomi watatu tofauti.
Amesema kwa jumla vikao hivyo vikiendelea kuahirishwa zaidi,vitamwathiri sana yeye pamoja na wapiga kura wake.
Naye wakili mwanadamizi wa serikali anayemsimamia mlalamikiwa wa pili ambaye ni mwanasheria mkuu wa serikali Vicent Tango, amesema yeye na wenzake wanaomsimamia mlalamikiwa wa tatu msimamizi wa uchaguzi, hawana pingamizi lolote dhidi ya ombi la wakili msomi Wasonga lililotokana na kuugua kwake.
Akitoa maamuzi yake Jaji Mzuna amesema mahakama yake kwa kuzingatia ubinadamu, kwamba mtu hawezi kufanya kazi vizuri kama afya yake sio nzuri, kwa hiyo mahakama hii itaendelea na vikao vyake .
Thursday, March 29, 2012

Home
SIASA
KESI YA SERUKAMBA YAFUTWA HUKU MAHAKAMA INAYOSIKILIZA KESI YA TUNDU LISSU MKOANI SINGIDA YAAHIRISHA KIKAO BAADA YA WAKILI KUUGUA GHAFLA.
KESI YA SERUKAMBA YAFUTWA HUKU MAHAKAMA INAYOSIKILIZA KESI YA TUNDU LISSU MKOANI SINGIDA YAAHIRISHA KIKAO BAADA YA WAKILI KUUGUA GHAFLA.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment