![]() |
Watoto
watatu waliojeruhiwa na Bomu katika Shule ya Msingi Kihinga wilaya ya Ngara
mkoani Kagera Novemba 2017 wakiagwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo Bw. Vedastus Tibaijuka (wa pili
kushoto) wakielekea KCMC kuwekewa macho bandia baada ya kampuni ya
Kabanga Nickel kugharimia Shilingi milioni 4 za matibabu yao .
Wa kwanza
kushoto ni Dkt Prosper Malya
na wengine ni Wazazi wa Watoto hao wanaowasindikiza katika matibabu yao.
|
![]() |
Mganga wa
Hospitali ya Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera Dkt Prosper Malya (kushoto) akiwasindikiza watoto watatu
waliojeruhiwa na bomu katika shule ya msingi Kihinga wilayani humo
Novemba mwaka jana wakielekea KCMC kuwekewa macho bandia baada ya kampuni
ya Kabanga Nickel kugharimia Shilingi milioni 4 za matibabu yao hapo May 24,
2018.
|
![]() |
Afisa Mahusiano
wa Kampuni ya Kabanga Nickel iliyoko wilaya ya Ngara mkoani Kagera Francis Wikedzi amesema kwamba Serikali
ya wilaya ilitoa maombi ya kusaidia watoto hao na kampuni
kama sehemu ya Jamii imetafuta wahisani wa ndani na nje ya wilaya na kupata
fedha za matibabu ya watoto hao.
Amesema
fedha hizo zitatumika kuwasafirisha watoto, wazazi wao na daktari
mmoja kutoka Hospitali ya Rulenge pamoja na Dereva kwenda na kurudi ambapo pia
zimeambatanishwa na gharama za matibabu kwa siku watakazoishi Hospitali ya KCMC.
|
![]() |
Januari
mwaka huu (2018) kampuni hiyo ilitoa msaada wa dawa zilizotumika kuwatibu
majeruhi katika Hospitali ya Rulenge na kutoa pia vifaa vya kujifunzia na sare
za wanafunzi 192 wa shule hiyo huku familia zilizopoteza watoto watano
zikipata ubani wa chakula vyote vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 20.7.
Katibu
tawala wa wilaya ya Ngara Vedastus
Tibaijuka kwa niaba ya Serikali ametoa pongezi kwa Kampuni ya Kabanga
Nickel kwa msaada huo na Taasisi ya Tumaini
Fund ambayo ilitoa Shilingi milioni 5 kuwatibisha majeruhi
waliotibiwa Hospitali ya Kagondo wilayani Muleba kwa watoto watatu
waliokuwa wamejeruhiwa miguu yao.
Aidha
Tibaijuka aliwashukuru pia Tumain Fund
kwa kugharimia matibabu ya majeruhi 42 waliolazwa Hospitali ya Rulenge na
kushukuru jamii iliyoguswa na tukio hilo kwa kuchangia damu, mavazi vyakula na
huduma nyinginezo.
|
No comments:
Post a Comment