Taswira Lori likikwama Darajani -Nyabibuye,Kakonko Kigoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 24, 2018

Taswira Lori likikwama Darajani -Nyabibuye,Kakonko Kigoma.

Lori hili lilikutwa limekwama Daraja la Kijiji cha Nyabibuye wilayani Kakonko mkoani Kigoma hivi Karibuni ambapo Wasafiri na Magari mengine ilibidi walazimike kusubiria kusombwa kwa magunia ya tangawizi yaliyokuwa yamo ndani ya Lori hilo ili kulinasua na kupata njia ya kupita.

Aidha barabara nyingine iliyo na usumbufu ni ile ya kutoka Mukalunzi kwenda Murusagama  wilayani Ngara mkoani Kagera ambako daraja limerundwa kwa mfumo wa mawe na magari yanayopita ni yenye tani moja lakini malori ya mizigo yakipita kuna hatari ya kutotoka ikiwa ni pamoja na barabara ya kutoka Murusagamba kuelekea daraja linalotenganisha wilaya ya Ngara na Kakonko.

Picha Na- Shaaban Ndyamukama.


Vijana wa kijii cha Nyabibuye wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wakihamisha magunia ya Tangawizi kutoka kwenye  Lori ambalo lilishindwa kupita kwenye daraja la kijiji hicho hivi karibuni kutokana na wingi wa magunia na barabara kudidimia  ikiwa kwenye matengenezo . 

Magunia ya Tangawizi yalikuwa yakisafirishwa kutoka  wilaya ya Kasulu mkoani humo hadi mkoa wa Muyinga nchini Burundi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad