Simba SC na Zawadi ya Milioni 100 za SportPesa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 24, 2018

Simba SC na Zawadi ya Milioni 100 za SportPesa.

Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa, Pavel Slavkov, (kushoto) akiwakabidhi hundi ya Sh. milioni 100, viongozi wa Simba na Nahodha wao John Bocco.

Wekundu wa Msimbazi Simba SC Leo May 24, 2018 imekabidhiwa kitita cha Shilingi milioni 100 kutoka kampuni ya SportPesa Ltd ikiwa moja ya fedha walizoahidiwa na kampuni  hiyo wakichukua Ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mujibu  wa mkataba walioingia nayo kama wadhamini wao wakuu.

 Hafla ya makabidhiano ya kitita hicho imefanyika kwenye ofisi za SportPesa zilizopo maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam huku ikihudhuriwa na viongozi wa pande zote mbili sambamba na wachezaji wa Simba SC wakiongozwa na nahodha wao John Bocco ambaye alifanya zoezi la kukabidhi kombe kwa wadhamini hao.
Nahodha wa Simba John Bocco (kulia) akimkabidhi kombe la ubingwa Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa, Pavel Slavkov, huku viongozi wengine kutoka Simba na kampuni hiyo wakishuhudia.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Kaimu Makamu wa Rais wa Simba, Iddi  Kajuna, alisema kuwa: “Tunaishukuru sana SportPesa kwa kututia nguvu tangu mwanzo wa Ligi hadi leo  hii ambapo wametukabidhi hundi hiyo ya shilingi milioni 100, bila kujali hata kuwa bado tuna mchezo mmoja ili tukamilishe ratiba yetu.

Pia tunawashukuru SportPesa kwa kutuwezesha kulipa mishahara ya wachezaji wetu mapema, jambo ambalo tunaamini kwa namna moja au nyingine limechangia kwa kiasi kikubwa kwetu kuibuka mabingwa wa Tanzania kwani bila kutoa mishahara kwa wakati yawezekana  leo hii tusingeweza kufikia malengo yetu,” alisema Kajuna.
Baadhi ya wachezaji wa Simba SC na makocha wa timu hiyo wakiwa ndani ya Ofisi za SportPesa.
Wachezaji na viongiozi wa Simba SC na SportPesa wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas akizungumza jambo kabla ya makabidhiano ya hundi hiyo kufanyika Leo May 24,2018.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema: “Kwa niaba ya kampuni yetu ya SportPesa nawapongeza sana Simba kwa kuwatendea haki mashabiki wa Simba kwani kufanya hivyo mmetupa heshima kubwa sana sisi wadhamini wenu wakuu, kwani mmeitendea haki sana nembo yetu kiasi cha kampuni yetu kuamini kuwa imefanya jambo muhimu kuwa wadhamini wenu wakuu,” alisema Abbas.
Kaimu Makamu wa Rais wa Simba SC Iddi Kajuna, akitoa neno la shukurani.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad