“Epukeni mazingira ya kujaribiwa kwa lengo la kuwasadia
watahiniwa; kama hamkuwafundisha vizuri waacheni washindwe, kwa sababu itakuwa
ndiyo haki yao.” Mkuu wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera,Lt. Col. Michael Mntenjele akitoa wito huo kwa
washiriki wa kazi maalumu Septemba 04, 2018.
Mkuu huyo wa
Wilaya ya Ngara Lt. Col. Mntenjele,
amesema watoto waliojifunza kwa bidii waachwe wafaulu kwa juhudi zao, huku
akiwataka washiriki wa kazi hiyo maalumu kuwa wautulivu, wenye akili pamoja na
busara.
“Hakikisheni sifa nzuri ya Wilaya ya Ngara inaendelea
kudumishwa, na kuhakikisha hakuna udanganyifu katika mithani kwa kusimamia vema
mtihani huu.” Alisema Lt. Col. Michael
Mntenjele.
Hata hivyo,
alisisitiza kwamba anatumaini washiriki hao, wataifanya kazi hiyo nyeti ya
kitaifa kwa uadilifu mkubwa, na kwa kuzingatia maelekezo ya kusimamizi mitihani
yaliyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
Aidha,
amesema uteuzi wa washiriki hao, umezingatia mwongozo na taratibu ambao
unasisitiza mshiriki lazima awe na sifa zinazokubalika, ambazo ni kuwa mwaminifu na mwadilifu, uzoefu kazini, afya njema, sifa za
kitaaluma pamoja na kufanya shughuli hii kwa kuzingatia maadili ya ualimu.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara na Mwenyekiti wa Kamati
ya Mitihani (W) Bw. Aidani John Bahama,
ametoa wito kwa wasimamizi wa mitihani wa darasa la saba mwaka huu 2018, kuwa
watulivu vituoni na kuacha tabia ya ulevi na vitendo viovu.
Amesema kuwa
Serikali haitamvumilia mtu anayeacha majukumu, huku akiwataka kuifanya kazi
hiyo kwa weledi na uaminifu mkubwa ili hata mwakani waweze kuteuliwa tena.
Kwa wilaya
ya Ngara mkoani Kagera kwa mwaka 2018 Jumla ya Watainiwa ni 5,095; watafanya Mtihani
wa Darasa la saba ulioanza leo September 5 hadi 6,2018 ,Wasichana wakiwa ni
2,644 na Wavulana ni 2,451.
Kati yao Watahiniwa
watatu wavulana wawili na msichana mmoja, wana uoni hafifu (Low Vision); ambapo
wavulana wanatoka shule ya msingi ya Ruganzo na msichana anatoka katika shule
ya msingi ya Muhweza.
|
No comments:
Post a Comment