Raundi ya 25 wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) - Simba SC yatakata kwa Tanzania Prisons. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 16, 2018

Raundi ya 25 wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) - Simba SC yatakata kwa Tanzania Prisons.

Emmanuel Okwi (kushoto) akishangilia na John Bocco (kulia) baada ya bao la kwanza leo April 16, 2018 na Kwa pamoja Bocco na Okwi wamefikisha magoli 33 msimu huu huku zikiwa zimebaki mechi sita kwenye Ligi.

Simba SC imezidi kuonesha kuwa ina kiu ya kuutwaa Ubingwa wa VPL 2017/2018 baada ya kuilaza Tanzania Prisons  mabao 2-0, katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo, Simba SC walipata bao la kwanza mnamo dakika ya 35 kupitia John Bocco aliyefunga kwa kichwa huku Kipindi cha pili , Simba  SC walipata penati katika dakika ya 80 baada ya John Bocco kudondoshwa eneo la penati na ikatumiwa vema na mshambuliaji Emmanuel Okwi kuandika bao la pili.

Matokeo hayo yameifanya Simba SC ifikishe pointi 58 baada ya kucheza mechi 24 za Ligi wakati Yanga SC ikiendelea kubaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 47, tofauti ya pointi 11 lakini Yanga SC imecheza mechi 22.


MATOKEO YA MICHEZO MINGINE YA VPL LEO.
John Bocco amefikisha magoli 14 na kufikia magoli ya Simon Msuva na Abdulrahman Mussa waliokuwa wafungaji bora wa msimu uliopita (2016/2017).

Emmanuel Okwi   kafunga goli la 19 kwenye Ligi msimu huu 2017/2018 na kumfanya afikie idadi ya mganda mwenzake Hamisi Kiiza ndani ya Simba SC lakini Okwi pia ameifikia rekodi iliyoiwekwa na Amis Tambwe wakati yupo Simba SC na Bocco wakati yupo Azam FC kufikisha magoli 19 kwa msimu mmoja.

MSIMAMO WA LIGI ULIVYOSASA BAADA YA RAUNDI YA 25 VPL. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad