Rais
Magufuli ameuambia mkutano wa 11 wa Baraza la Biashara la Taifa kuwa ni Viwanda
nane tu ikiwemo Kampuni ya Bakhresa ndivyo ambavyo vimekuwa havifanyi
udanganyifu.
Rais John
Magufuli leo Jumatatu, Machi 19 ameweka wazi matokeo ya kamati teule aliyoiunda
kuchunguza mwenendo wa viwanda vinavyoagiza sukari ya viwandani.
Rais
Magufuli ameuambia mkutano wa 11 wa Baraza la Biashara la Taifa kuwa ni viwanda
nane tu ikiwemo Kampuni ya Bakhresa ndivyo ambavyo vimekuwa havifanyi
udanganyifu.
"Viwanda
nane tu ndio safi, kuna baadhi ya viwanda vinakasoro ndogo ndogo ikiwemo
kuagiza sukari nyingi zaidi ya mahitaji yao...lakini wapo wenye matatizo
makubwa kabisa, vipo viwanda hewa kunakimoja kiliagiza tani 7,000 tukaambiwa
kipo Mbeya kwenda huko hakikukutwa, ni kiwanda hewa, mi nilijua kuna
wafanyakazi hewa tu, kumbe na viwanda pia vipo."
"Serikali
yangu wala haina nia ya kuwasumbua wazalishaji wanaotumia sukari hii kihalali,
lakini kwa mwenendo huu lazima tuwe macho ili sukari hii isiingie sokoni na
kuumiza walaji."
|
Katika hatua
nyingine,Rais John Magufuli ameeleza kuwa siku za hivi karibuni atakutana na
Wakurugenzi Watendaji wawili kutoka nchi za Ujerumani na Denmark ambao watakuja
kufanya uwekezaji nchini.
Rais
Magufuli ameeleza kuwa watakuja kufanya uwekezaji wa kiwanda kipya cha Petroli
Kemikali (Petrol Chemical Plant) ambacho kitakuwa na thamani ya Dola za
Marekani Bilioni 1.92 ambayo ni sawa na takriban Shilingi za Kitanzania
Trilioni 4.56.
Ameeleza
kuwa kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 4000 katika
eneo la Kilwa kwa ajili ya kutengeneza mbolea ambayo itauzwa ndani pamoja na nje
ya nchi kwa kutumia gesi iliyopo nchini.
|
No comments:
Post a Comment