Onyo la Naibu Waziri wa Elimu kwa Walimu Nchini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 02, 2018

Onyo la Naibu Waziri wa Elimu kwa Walimu Nchini.

Naibu Waziri wa Elimu William Ole Nasha jana March 1, 2018 alikuwa mkoani Mara katika ziara ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya shule inayoojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia programu ya lipa kulingana na matokeo (EP4R).

Katika ziara hiyo Ole Nasha ametoa onyo kwa walimu wote nchi wanaojihusisha  kimapenzi na wanafunzi na kuwaambia waache mara moja tabia ya kuwarubuni wanafunzi badala yake warudishe nidhamu ya wanafunzi na kuinua kiwango cha elimu na ufaulu katika shule wanazofundisha.

Ole Nasha amesema amepokea taarifa juu ya baadhi ya walimu kujihusisha kimapenzi na wanafunzi wao jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi pamoja na maadili ya utumishi wa umma.

Ameeleza kuwa serikali haitamvumilia mwalimu yeyote mwenye tabia kama hizo na kuongeza kuwa mwalimu atakayebainika kushiriki vitendo hivyo atashtakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi pamoja na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kulingana na taratibu za utumishi wa umma.

Pia amewataka wazazi na walezi kuhakikisha hawajihusishi kwa namna yoyote kupokea fedha ili kuwaficha wahalifu wanaokatiza masomo ya watoto wao kwa kuwapa ujauzito badala yake waache sheria ichukue mkondo wake ili kusaidia kukomesha vitendo hivi viovu katika jamii.

Nae Mkuu wa wilaya ya ya Musoma Dk Vicent Naano amesema wilaya yake inakabiliwa na tatizo la mimba za utotoni ambapo kwa mwaka wastani wa wanafunzi mia moja wanapata ujauzito na kukatiza masomo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad