Uzazi wa
mpango una mambo mengi sana.. sio kuzuia mimba tu ndio uzazi wa mpango ila hata
kupanga idadi na jinsia za watoto ni moja ya njia za uzazi wa mpango.
Watu wengi
wamekua wakitamani jinsia flani za watoto ili wazae watoto wachache ila kukosa
kwa jinsia waliyoipanga hujikuta wakizaa watoto wengi wakati wakitafuta jinsia
husika, mpaka familia hugombana na kutengana kwa sababu hizi.
Mara nyingi
wazazi wa kiume hufikia hatua ya kuvunja ndoa kabisa hasa wanapokosa watoto wa
kiume.
Kitaalamu
mbegu zinazotoa mtoto wa kiume XY huenda kwa mwendo mkali sana kwenda kwenye
mfuko wa uzazi lakini hufa haraka. lakini mbegu zinazotoa mtoto wa kike XX
husafiri taratibu na huchelewa kufika na kufa ndani ya mfuko wa uzazi kwani
mbegu hizi huweza kuvumilia hali mbaya ya kimazingira ndani ya mfuko wa uzazi
wa mwanamke, hivyo njia pekee ya kupata mtoto wa kiume ni kuhakikisha mbegu
hizo za kiumeXY zinakutana na mayai ya kike kwenye mfuko wa uzazi haraka kabla
ya kufa..
Zifuatazo ni
njia hizo tano kali…
1. Hakikisha unashiriki tendo la ndoa
siku mayai ya mwanamke yanapokua yameshuka{ovulation}
Ukishiriki
tendo la ndoa siku hii ambayo yai linakua limeshuka mbegu za kiume huweza
kufika mapema na kujiunga na mayai ya kike na kutengeneza
mtoto{fertilization}hii ni siku ya 14 KABLA YA KUONA DAMU YA MWEZI UNAOFUATA
SIO BAADA YA KUONA SIKU ZAKO..
Kama wewe
mwanamke hujui siku yako ya ovulation fanya hivi.
Pima joto
lako la mwili: nunua kipima joto[thermometer} na kisha pima joto lako kila
asubuhi , siku ukiona joto lako limeongezeka kidogo ujue umeanza ovulation na
hiyo ndio siku muhimu ya kutafuta mtoto..
Angalia maji
maji ya uke: kawaida maji ya uke hua mazito na kuvutika kama maji ya mayai
mabichi wakati mwanamke anapoanza ovulation..
2. Wewe mwanaume ongeza idadi ya
mbegu zako..{sperm count}
Mwanaume
anatakiwa aongeze wingi wa mbegu zake hasa kwa kukaa siku mbili mpaka tano bila
kushiriki tendo la ndoa wakati akisubiri mwanamke wake aanze ovulation.
Njia zingine
za kuongeza mbegu ni weka korodani kwenye hali ya ubaridi:
kawaida
korodani hutengeneza mbegu nyingi wakati wa hali ya ubaridi kuliko joto hivyo
mwanaume anatakiwa kuepuka kuvaa nguo zilizobana sana, na kuwekalaptop kwenye
mapaja acha kuvuta sigara na kunywa pombe:wanaume wanaokunywa pombe na kuvuta
sigara hua na mbegu kidogo sawasawa na wavutaji wa bangi.. matumizi ya dawa za
cancer pia husababisha uzalishaji wa mbegu kidogo sana.
3. Tumia style za ngono ambazo
zinahamasisha muingilio mkubwa{deep penetration}
Hii huzipa
faida mbegu za mtoto wa kiume{XY} kufika haraka na kufanya fertilization na
upande mwingine, muingiliano mdogo{shallow penetration}husababisha mbegu
kumwagwa mbali na mlango wa mfuko wa uzazi hivyo mbegu huweza kukutana na hali
ya tindikali kwenye uke hivyo mbegu za mtoto wa kiume kufa haraka na kuziacha
mbegu zinazotoa mtoto wa kike.{XX}.
4. Hakikisha mwanamke anafika
kileleni:
Mwanamke
anapofika kileleni hutoa maji mengi ukeni ambayo hupunguza wingi wa tindikali
ambayo ni adui wa mbegu zote hasa mbegu za mtoto wa kiume XY ambazo hua
haziwezi kuvumilia hali ngumu ya kimazingira.
5. Usifanye tendo la ndoa kabla na
baada ya Ovulation;
Kabla ya
ovulation mbegu za mtoto wa kiume XY hufika haraka kwenye mfuko wa uzazi kama
kawaida na kukuta mayai ya mwanamke hayajafika na kufa vivo hivyo baada ya
ovulation.
|
Monday, March 12, 2018
Njia za Kisayansi itakayokupelekea Kupata Mtoto wa Kiume.
Tags
# DONDOO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
DONDOO
Labels:
DONDOO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment