Muonekano wa
chupa za plastiki zilizokusanya mtaani
na kuhifadhiwa hapa eneo moja Rusumo,wilayani Ngara mkoani Kagera.
|
Hakika zamani
ilikuwa ni laana kuambiwa utaokota Makopo. Siku hizi ni fursa ya Biashara
inayokuza kipato cha wote wanaoweza kufanya hivyo.
|
Kutokana na
maendeleo ya kiuchumi na ongezeko la uhaba wa ajira rasmi, hivi sasa kuna
Wanawake, Vijana hata Wazee, wanaookota Chupa hizi kujipatia Kipato.
|
Kwa Mujibu
wa Kiwanda cha Oak Hall cha Marekani kinachozitumia kuzalisha Nguo za aina
mbalimbali, Chupa 27 zinatosha kutengeneza Joho Moja.
|
Kama ilivyo
kwa Biashara nyingine, Changamoto hazikosekani. Wataalamu wa Afya wanasema
umakini unahitajika kwa wote wanaojihusisha na Biashara hii hasa waokotaji.
|
Kwa mtazamo,
Biashara ya chupa imesaidia kuimarisha usafi wa maeneo mengi nchini.
Maeneo mengi
sasa zaidi ya watu wanajishughulisha na uokotaji taka hivyo kupunguza kuzagaa
kwake mtaani kwa kuziona ni fursa.
|
No comments:
Post a Comment