WATU wengi
hulitumia tunda la papai kwa sababu ya utamu wake lakini lina faida lukuki kwa
afya ya Mwanadamu.
Tunda la
papai lina vitamini A,B,C,D, na E jambo linaloliweka tunda hili katika kundi la
matunda na vyakula vyenye utajiri mkubwa wa vitamini.
Inaelezwa
kwamba, kutokana na uzuri wa tunda hili, mvumbuzi maarufu anayeaminika
kulivumbua Bara la Amerika, Christopher Columbus, alilipachika papai jina la
‘Tunda la Malaika’.
Mbegu za
papai huliwa pia, ingawa zina ladha chungu, lakini hazina madhara bali zina
faida kiafya.
Tunda na
mbegu zina aina pekee ya kimeng’enyo (enzymes) kiitwacho Papain, ambacho ni
muhimu katika kusaidia usagaji wa protini mwilini pia hutumika kama dawa
mwilini ya kutibu majeraha kwenye utumbo na matatizo mengine.
Kimeng’enyo hicho
hupatikana kwa wingi pale papai linapokuwa bado bichi. Kwa kawaida mapapai
mabichi lakini
yaliyokwisha
komaa vizuri, ndiyo hutumika kupata virutubisho hivyo ambavyo hutengenezwa
vidonge vya lishe (Food Suplements).
Papai ni
chanzo kikuu cha virutubisho vinavyotoa kinga kubwa ya mwili (antioxidants)
kama vile Carotenes, Vitamini C, Flavonoids na jamii zote za Vitamin B. Mbali
ya kuwa na Vitamini, papai pia lina madini ya Potassium, Magnesium na Fiber.
Virutubisho
vyote hivyo vina kazi kubwa mwilini ya kuimarisha utendaji kazi mzuri wa mfumo
mzima wa moyo na kutoa kinga kubwa dhidi ya ugonjwa wa saratani ya utumbo.
Hivyo ulaji wa tunda hili, ni tiketi ya uhakika ya kwenda mbali na matatizo ya
moyo na saratani ya utumbo.
Vile vile
papai linaweza kuwa na msaada mkubwa katika kuzuia kisukari kutokana na kuwa na
kiwango kikubwa cha vitamini C, E na A, vitamani ambazo zina nguvu na ni muhimu
sana katika kutoa kinga dhidi ya magonjwa hayo. Vitamini hizo pia ndizo
zinazozuia ile hali ya kuganda mwilini
kwa mafuta aina ya Cholestrol (Oxidation of Cholestrol).
Cholestrol
inapoganda, ndipo inapokuwa na uwezo wa kukwama na kujikusanya kwenye kuta za
mishipa ya damu na kuanza kutengeneza uzio hatari ambao husababisha mshituko wa
moyo au kiharusi.
Njia pekee
ya kupambana na hali hiyo isitokee mwilini mwako ni kula kwa wingi papai lenye
kiwango kikubwa cha vitamin E na C ambazo ndizo zinazodhibiti kuganda kwa
mafuta mabaya na mazuri ya Cholestrol.
Papai pia
lina kirutubisho kingine muhimu aina ya Fiber (ufumwele) ambacho kimeonesha
uwezo mkubwa wa kushusha kiwango cha Cholestrol mwilini.
Umuhimu wa
kirutubisho aina ya Fiber, kilichomo kwenye papai, ni mkubwa kama vile kusaidia
usagaji wa chakula tumboni hivyo kumuwezesha mtu kupata choo laini, na
kirutusho hiki kimeonesha uwezo wa kutoa kinga dhidi ya saratani ya utumbo
ambayo huwa na uhusiano mkubwa wa mtu kukosa choo kwa muda mrefu au kupata kwa
tabu.
Virutubisho
vyote vilivyomo kwenye papai hutoa kinga ya pamoja kwenye chembe hai za utumbo
dhidi ya vijidudu nyemelezi. Hivyo kwa kuongeza ulaji wa tunda hili, unakuwa
unajipa kinga madhubuti dhidi ya magonjwa tuliyoyataja hapo juu.
Makala haya yameandaliwa na Mtaalam
wa lishe, Abdallah Mandai, pia kwa ushauri wasiliana naye kwa simu 0754 391 743
au 0717 961 796.
|
Tuesday, March 20, 2018
Zifahamu Faida za Kula Papai.
Tags
# DONDOO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
DONDOO
Labels:
DONDOO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment