Yanga SC yala sahani moja na Simba SC katika mbio za Ubingwa, ikishinda goli 5-0 dhidi ya Mbeya City. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, November 19, 2017

Yanga SC yala sahani moja na Simba SC katika mbio za Ubingwa, ikishinda goli 5-0 dhidi ya Mbeya City.

Mchezaji Obrey Chirwa akiinua mikono kuwapigia makofi mashabiki wa Yanga SC baada ya kufunga mabao matatu  Leo November 19, 2017 katika uwanja wa Uhuru ambao ndio wanautumia kama uwanja wao wa nyumbani na wamefanikiwa kupata ushindi mnono wa magoli 5-0 dhidi ya Mbeya City.

Hat-trick ya mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa ni ya pili kwenye ligi kuu Tanzania bara baada ya Emanuel Okwi kufanya hivyo (Okwi alifunga goli 4) kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi August 26, 2017 Simba ilipocheza dhidi ya Ruvu Shooting.

Katika huo mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2017/2018 Yanga SC sasa inafikisha pointi 20, ikizidiwa Pointi mbili na vinara Simba SC na Azam FC baada ya timu zote za Dar es Salaam kucheza mechi 10 za Ligi Kuu msimu huu. 

Shujaa wa ushindi wa Yanga SC leo ni mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa aliyefunga mabao matatu peke yake, wakati mabao mengine mawili yalifungwa na chipukizi Emmanuel Martin.

MATOKEO YA MECHI ZINGINE ZA LEO JUMAPILI.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad