Rais Mugabe Avuliwa Uongozi Ndani ya ZANU PF. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, November 19, 2017

Rais Mugabe Avuliwa Uongozi Ndani ya ZANU PF.

Chama cha ZANU PF cha Zimbabwe kimemvua uongozi wa Chama hicho, Rais Robert Mugabe na kumchagua aliyekuwa Makamu wa Rais, Bw.Emmerson Mnangagwa kukiongoza ambaye alifutwa wiki mbili zilizopita kama kiongozi wake.

Kufutwa kwa Bw. Mnangawa kumezua mambo mengi huku Jeshi likitwaa madaraka na kumzuia Mugabe miaka 93, kumteua mke wake Grace kama makamu wa Rais.

Wazimbabwe Jana Jumamosi Novemba 18,2017 walishiriki maandamano kupinga utawala wa Rais Mugabe ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 30 sasa.
Maelfu ya raia wa Zimbabwe jana walijitokeza barabarani hasa mjini Harare katika jitihada za kuongeza shinikizo za kumtaka rais Mugabe ajiuzuulu.

Rais Mugabe anatarajiwa kukutana na viongozi wa jeshi la nchi hiyo na tayari msafara wa magari umeonekana ukitoka nyumbani kwake.

Kiongozi wa chama cha maveterani wa vita ya ukombozi wa Taifa hilo, Chris Mutsvangwa ameliambia Shirika la Habari la Reuters kwamba, chama hicho pia kimeanza mchakato wa kumwondoa Mugabe kama Rais wa nchi hiyo.

Reuters imeripoti kwamba Grace, mkewe Mugabe amefukuzwa uanachama.

Watu wameonekana mitaani wakicheza na kushangilia baada ya ZANU PF kumwondoa katika uongozi Mugabe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad