Msimamo wa Makundi ya UEFA Champions League 2017/2018. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 22, 2017

Msimamo wa Makundi ya UEFA Champions League 2017/2018.

Cristiano Ronaldo akifurahia  bao baada ya kuifungia Real Madrid bao la sita dakika ya 54 katika ushindi wa Goli 6-0 dhidi ya wenyeji, APOEL kwenye mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya 2017/2018 usiku wa Jana November 21,2017 Uwanja wa Neo GSP mjini Nicosia nchini Cyprus.

 Ronaldo alifunga mabao mawili, lingine dakika ya 49, wakati mabao mengine ya Real Madrid yalifungwa na Luka Modric dakika ya 23, Karim Benzema mawili dakika za 39 na 45 na ushei na Nacho dakika ya 42 

Michezo kadhaa ya klabu Bingwa barani Ulaya ilipigwa usiku wa Jana pia November 21,2017, Liverpool walitoka sare ya mabao 3 - 3 dhidi Sevilla, Manchester City wakiendeleza makali yao baada ya kutoka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Feyenoord, wakati Tottenham nao wakiibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Dortmund.

Na huu ndiyomsimamo wa makundi unavyoonyesha baada ya michezo ya hapojana siku ya Jumanne kumalizika.

Kundi A, linaongozwa na Manchester United yenye alama 12, ikifuatiwa na FC Basel yenye pointi 6 na nafasi ya tatu ikishikwa na CSKA Moscow yenye alama 6.

Kundi B, linaongozwa na Paris Saint Germain wenye alama 12, ikifuatiwa na Bayern Munich wakiwa na alama 9 na nafasi ya tatu ikishikwa na Celtic wakiwa na pointi 3.


Kund C, ikiongozwa na Roma wenye alama 8, ikifuatiwa na Chelsea wenye pointi 7 na nafasi ya tatu ikishikwa na Atletico Madrid wakiwa wamejikusanyia alama 3.

Kundi D, linaongozwa na Barcelona kwakuwa na alama 10, nafasi ya pili ikishikwa na Juventus wenye pointi 7 na ya tatu wakishika Sporting Lisbon wenye alama 4.

Kundi E, Liverpool inaongoza kwa kuwa na alama 9, ikifuatiwa na Sevilla wenye pointi 8 na watatu katika kundi hilo ni timu ya Spartak Mosco wenye alama 6.

Kundi F, Manchester City inaongoza kwa kuwa na alama 15 ikifuatiwa na Shakhtar Donetsk wenye point 9 na ya tatu ni Napoli ikiwa na alama 6.

Kundi G, Besiktas inaongoza kwa kuwa na alama 11, nafasi ya pili ikishikiliwa na FC Porto wenye pointi 7 na ya tatu ni RB Leipzing wakiwa na alama 7.

Kundi la mwisho ni H, likiongozwa na Totteham Hotspur wakiwa na pointi 13, Real Madri alama 10 na Borussia Dortmund wenye pointi 2.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad