Msanii Nikki
wa Pili ambaye ni miongoni mwa wasanii wasomi nchini, ameitwa kujiunga na chama
cha ACT Wazalendo, ili kuongeza nguvu na kukijenga zaidi chama hiko.
Kiongozi wa
chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amemuandikia ujumbe kwenye ukurasa
wake wa twitter kumuomba kufanya hivyo.
"Njoo ujenge Chama
cha kijamaa bana acha mambo yako", ameandika Zitto Kabwe kwenye ukurasa wa Nikki wa
pili.
Baada ya
tweet ya Zitto Kabwe kumuomba Nikki, Nikki alimjibu kuwa chama cha kijamaa
kinajengwa na watu wanyonge, bali yeye
kama mtu wa vyombo vya habari sio wa kuaminika kwani hawachelewi
kuwauza.
"Chama cha kijamaa
hujengwa na vugu vugu la wanyonge wenyewe, ni muwe tu na mkakati wa
kuwaunganisha ki ideologia, umoja zao hizo za boda boda, machinga, wakulima,
sisi watu wa media hatu kawii kuwauza sokoni kama nyanya", ameandika Nikki wa Pili.
Mpaka sasa
haijulikani msanii huyo ni mfuasi wa chama gani kutokana na kuonekana kuwa
mwanaharakati wa masuala ya kisiasa na uchumi, na hajawahi kuonekana kwenye
jukwaa la chama chochote kufanya kampeni.
|
No comments:
Post a Comment