Emmerson Mnangagwa Rais mpya wa Zimbabwe Aapishwa jijini Harare. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, November 24, 2017

Emmerson Mnangagwa Rais mpya wa Zimbabwe Aapishwa jijini Harare.

Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wakati wa kuapishwa kwake, Harare November 24,2017.

Hatimaye Rais mpya wa Zimbabwe,Bw. Emmerson Mnangagwa ameapishwa rasmi kuchukua wadhifa huo kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe siku ya Jumanne wiki hii kwa shinikizo la Jeshi na Chama chake cha Zanu-PF.

Mnangagwa ameapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla.
Bw.Mnangagwa ameshangaliwa na maelfu ya raia wa nchi hiyo waliofika kushuhudia mabadiliko ya uongozini nchini humo, kufuatia kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla.

Amesema kuwa licha ya makosa yaliofanywa na Mugabe ni muhimu kukubali na kutambua mchango wake kuhusu ujenzi wa taifa.

Amesema kuwa mabadiliko ya umiliki wa ardhi yalifanyika na hayawezi kubadilishwa kwa kuwa huo utakuwa ukiukaji mkubwa wa upiganiaji wa Uhuru.

Lakini rais huo mpya ameahidi kuwalipa wakulima waliopoteza mashamba yao katika sera tata iliotekelezwa na utawala wa rais Mugabe.

Baada ya rais huyo mpya kuapishwa, mizinga 21 ilipigwa kumkribisha Rais Emmersonn Mnangagwa.

Umati wa watu ulipiga kelele kufuatia hatua ya jeshi kupiga hewani risasi 21 kama heshima za kumkaribisha rais mpya.
Bw. Mnangagwa aliapa kulinda haki za raia wa Zimbabwe.

Upinzani unamtaka rais Mnangagwa kuwa tofauti na mtangulizi wake na kudumish ademokrasia kwa taifa hilo lililojipatia uhuru wake mwaka 1980.

Mbali na raia wa Zimbabwe, viongozi wengine wa Afrika wanashuhudia mabadiliko hayo akiwemo rais wa Zambia Edgar Lungu na Ian Khama wa Bostwana.

Rais wa zamani Zambia Keneth Kaunda na Rupia Banda nao pia wamehudhuria sherehe hizo jijini Harare.

Emmerson Mnangagwa ataongoza Zimbabwe kwa kipindi cha miezi nane hadi kuelekea uchaguzi mwaka ujao, na tayari chama chake cha Zanu-PF kilimteua hivi karibuni kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa urais mwaka ujao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad