DC Mtenjele - ''Wanangara acheni Kutengana'' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, October 07, 2017

DC Mtenjele - ''Wanangara acheni Kutengana''

Wakazi wa wilaya ya Ngara  mkoani Kagera wametakiwa kuacha mara moja mchakato wa kutengana kwa kutaka Jimbo Jipya la Uchaguzi na kubaguana kiukabila kati ya Washubi na Wahangaza na kudumaza  shughuli za Maendeleo na Kiuchumi.

 Mkuu wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mtenjele amesema hayo leo October 7, 2017  wakati akihutubia Wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM wa wilaya hiyo wa kuchagua viongozi mbalimbali wa chama hicho watakaodumu madarakani hadi mwaka 2022.

Luteni Kanali Mntenjele amesema Serikali haina mpango wa kugawa maeneo ya kiutawala na wakazi wa Ngara wapoteza ndoto za kuwa na Majimbo mawili ya Ngara Kaskazini na Kusini na kuendekeza ukabila wa Wahangaza kutoka  Ngara Kaskazini na Washubi walioko ukanda wa Ngara kusini.



Amesema kitendo cha kuendekeza maeneo ya utawala wa Bushubi na Bugufi kutawasababisha wasipate Maendeleo ya haraka katika kukabiliana na changamoto za umaskini na vikwazo vya kiuchumi wakihitaji Serikali kuboresha huduma za kijamii.

Rais Magufuli akiwa ziara ya kukutana na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza wilayani Ngara  mwezi Agost mwaka huu 2017 alisisitiza kuacha utengano na kuendekeza ukabila wa kikanda katika kuwapata viongozi wawakilishi wa wananchi katika ngazi za chama na serikali.

Katika mkutano huo wa uchaguzi Mkuu wa CCM,Wagombea watatu wa   nafasi ya Mwenyekiti  wa wilaya ya Ngara  ni pamoja na Hadson Bagege anayetetea kiti chake, George Rubagola  na Joseph Bihume. 


Mkutano wa uchaguzi wa CCM wa wilaya hiyo umehudhuriwa na wajumbe 512 kwa ajili ya  kuwachagua  viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya wilaya hadi  mkutano mkuu wa Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad