Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza
mabadiliko madogo katika baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo
Oktoba 7, 2017.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim
Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na maafisa
waandamizi wa Ofisi ya Rais walikuwapo. Taarifa kamili itawajia baada ya muda
si mrefu.
Picha na Ikulu.
Rais wa
Tanzania ,Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri
nchini huku akizigawanya baadhi ya Wizara zikiwemo Wizara ya Kilimo
na Mifugo, Nishati na Madini na kuongeza
Wizara mpya mbili na kufikisha Jumla ya Wizara 21.
Katika
Mabadiliko hayo, Mawaziri wawili na Manaibu Waziri wameongezwa.
Aidha Rais
Magufuli ametangaza mabadiliko na kuteua Katibu mpya wa Bunge huku akieleza
kuwa aliyekuwa Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila atapangiwa kazi nyingine.
Kwa
ufupi.
Mhe.Mahiga,
Mhe.Mwakyembe, Mhe.Kabudi, wamendelea na Wizara zao.
Katibu wa Bunge: Aondolewa na kuwekwa mpya
Mhe.Medadi Kalemani: Wizara ya Madini (imegawanywa kwa sasa)
Mhe.Angela Kairuki: Waziri wa Nishati na Madini.
HAPA TAZAMA
KWA KUPLAY VIDEO RASI MAGUFULI
AKITANGAZA MAWAZIRI LEO OCTOBER 07,2017.
|
No comments:
Post a Comment