Taswira Picha Mwenge wa Uhuru ulivyozindua Miradi Kata ya Kasulo,wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 02, 2017

Taswira Picha Mwenge wa Uhuru ulivyozindua Miradi Kata ya Kasulo,wilayani Ngara mkoani Kagera.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Baramba wakiupokea Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili shuleni hapo leo August 2,2017.

Mwenge wa Uhuru umewasili wilayani Ngara mkoani Kagera ukitokea wilayani Biharamulo ambapo Ukiwa wilayani Ngara,utapitia miradi 11 ya Maendeleo yenye thamani ya Tsh 4.5 Bilioni.
Ukiwa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Baramba , kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2017, Bw. Amour Hammad Amour amezindua bweni la wanafunzi wa shule hiyo na kufungua klabu ya kuzuia na kupambana na rushwa katika shule hiyo leo hii August 2, 2017.
Picha ya pamoja ,Viongozi  wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw.Michael Mtenjele ,Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Baramba sambamba na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2017, Bw. Amour Hammad Amour ulipowasili shuleni hapo kuzindua bweni la wanafunzi wa shule hiyo na kufungua klabu ya kuzuia na kupambana na rushwa katika shule hiyo leo hii August 2, 2017.

Hapa ni Kata ya Kasulo.

Uzinduzi wa tanki la kuhifadhia maji katika Kata ya Kasulo wilayani Ngara wakati wa mbio za Mwenge 2017. Tanki hili limegharimu jumla ya Tsh. 42,334,000.00 na lina ujazo wa Lita 120,000. Mradi huu husimamiwa na kamati ya kikundi cha mradi wa maji cha BENGUKA (Benaco Nguvu Kazi).

Katika kata ya Kasulo (Benaco) Mwenge wa Uhuru umezindua miradi mikubwa mitatu ya maendeleo yenye thamani ya Tshs. 296,714,400/= .
Picha juu na chini ni Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2017, Bw. Amour Hammad Amour akipanda mti wa kumbukumbu ikiwa ni ishara ya kutunza mazingira mara baada ya kuwasili  Shule ya Sekondari ya Wasichana na Baramba kuzindua bweni la wanafunzi wa shule hiyo na kufungua klabu ya kuzuia na kupambana na rushwa katika shule hiyo leo hii August 2, 2017.

Post Bottom Ad