Pamoja na serikali kuongeza uwekezaji katika
sekta ya elimu, ikiwa ni asilimia 17 ya bajeti nzima, mazingira ya kufundisha
na kufundishwa nchini bado si mazuri.
Akiwasilisha mada kuhusu bajeti ya elimu baada
ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa
ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo Dk Joviter Katabaro kutoka
Skuli ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam pamoja na kuwekwa maeneo ya
kuangaliwa kwanza ipo haja ya kufanya zaidi ili kufikia malengo.
Dk Katabaro katika mada yake alisema kwamba
pamoja na serikali kutenga zaidi ya TZS 1.366,685,241,000.00 katika
Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi huku Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na
Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) ikipatiwa sh 201,655,446,000/- kwa ajili ya elimu,
alisema kwamba anaona ipo haja ya kuongeza nguvu katika maeneo kadhaa ili
kuweka sawa mazingira ya kufundisha na kufundishwa.
Katika mjadala huo wa kitaifa uliodhaminiwa na
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Katabaro alisema kwamba kwa
sasa vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinakosekana katika shule nyingi na
taasisi zinazohusiana na elimu na hivyo kukwamisha ufanisi na tija katika
elimu.
Aidha katika mada yake alitaka juhudi
inayofanywa ya kuweka sawa mizania ya walimu pale walipo wengi kuhamishwa
inabidi iendelee ili kuweka uwiano sawa wa elimu nchini.
Pia alisema kuwa uwiano wa sasa wa walimu
nchini sio sawa huku katika masomo, baadhi yakiwa na walimu wa ziada na mengine
yakiwa na upungufu mkubwa.
|
Mkuu wa Utawala na Maendeleo ya Uwezeshaji wa
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la
ukaribisho kwa washiriki wa kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya
bajeti ya serikali 2017/2018 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwaka 2016 kwa mujibu wake kulikuwa na
walimu wa ziada katika masomo kadha huku kukiwa na upungufu katika masomo
mengine hasa Hesabu na Sayansi: Basic Mathematics – 7,291 (Upungufu);Biolojia –
5181 (Upungufu);Kemia – 5373 (Upungufu);Fizikia – 6873 (Upungufu);Kilimo 508
(Upungufu);Kingereza– 1267 (ziada); Jiografia – 3281 (ziada); Historia – 4764
(ziada) na Kiswahili – 4795 (ziada).
Pamoja na masomo Dk. Katabaro aliangalia
bajeti hiyo katika maeneo muhimu yanayofanya mtoto kuwa na akili kama viwanja
vya michezo na upatikanaji wa maji safi kwa ajili ya kunywa na usafi.
Maji haya ni muhimu sana kwa watoto wa kike
ambao usafi wao ndio siri ya mahudhurio ya shule kila siku.
|
Profesa wa Menejimenti ya Elimu kutoka Skuli
ya Elimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Eustella Bhalalusesa (katikati)
akifafanua jambo kabla ya kumkaribisha muwasilisha mada (hayupo pichani) kuhusu
bajeti ya elimu baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la
majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/2018 katika elimu na kilimo
lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mada hiyo pia ilitahadharisha kuhusu takwimu
ikitaka zitumike vyema ili kuondoa mipango mibovu hasa ya uandikishaji wa
watoto wa darasa la kwanza na wale wanaoingia kidato cha kwanza.
Wakati huo huo katika mada iliyowakilishwa kwa
pamoja kati ya Profesa haidari Amani na John Shilinde, kilimo pamoja na
kutegemewa na wengi na kuwa chachu ya maendeleo ya viwanda bajeti yake
iliyotengwa bado ni ndogo.
Walisema kwamba sekta hiyo ilipata kiasi cha
karibu asilimia 10 ya bajeti nzima, bajeti ambayo ukiiangalia utaona kwamba
haiwezi kubadili kilimo.
Wamesema kwamba kilimo ambacho huajiri
asilimia 70 ya wananchi ikichangia asilimia 28 ya pato la taifa huku ikipatia
asilimia 30 ya mapato ya kigeni na kuchangia asilimia 65 ya mali ghafi, bado
sekta haijapewa nguvu za kutosha kusonga mbele.
Wamesema kilimo kitabadilika kwa fedha za
utafiti na sayansi na ubunifu ili kuiweka sekta katika hali bora zaidi.
Walisema kwamba sayansi na ubunifu ni
kichocheo kikubwa cha mabadiliko katika kilimo.
Wataalamu hao walitaka bajeti zaidi kwa ajili
ya utafiti na maendeleo, kilimo cha umwagiliaji, kuongeza ruzuku, kuboresha
kilimo cha kisasa cha kutumia zana kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno,
kuongeza kazi zenye staha vijijijni, kuongeza mnyororo wa thamani na matumizi
endelevu ya ardhi na maji.
|
Pichani juu na chini ni sehemu ya wadau wa
kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/2018
katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam.
|
Picha ya pamoja ya wadau walioshiriki kwenye
kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/2018
katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam.
|
No comments:
Post a Comment