Taswira Picha Shabiki wa Man United na Wayne Rooney walivyokumbatiana Uwanjani. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 14, 2017

Taswira Picha Shabiki wa Man United na Wayne Rooney walivyokumbatiana Uwanjani.

Shabiki mmoja Pichani ameshindwa kujizuia baada ya kutoka jukwaani na kuingia hadi uwanjani kwenda kumkumbatia Mchezaji wa Everton, Wayne Rooney wakati wa mechi ya kirafiki kati ya Gor Mahia dhidi ya Everton.

Mechi hiyo imemalizika kwa Everton kupata ushindi wa magoli 2-1. Everton walitangulia kufunga goli la kwanza ambalo lilipachikwa na Rooney kisha Medie Kagere akaisawazishia Gor Gor Mahia kabla ya Dowell kufunga bao la pili kwa Everton.

Jamaa huyo ambae alikuwa amevaa jezi ya Manchester United , alikimbia kutoka jukwaani na kukatiza uwanjani hadi kwa Rooney mwenye umri wa miaka 31, alifunga bao zuri kwa shuti la umbali wa mita 30 dakika ya 34 na kumkumbatia.
Rooney na wachezaji wenzake wa Everton baada ya kuisaidia timu hiyo kuilaza Gor Mahia ya Kenya.

Wayne Rooney aliyerejea Everton wiki iliyopita baada ya miaka 13 tangu ahamie Manchester United amekumbushia kitu alichofanya wakati anajiunga na timu hiyo ya Merseyside kwa mara ya kwanza kabisa alipofunga bao lake la kwanza katika mechi ya kwanza dhidi ya Arsenal mwaka 2002, siku tano kabla hajatimiza miaka 17.

Timu ya Gor Mahia ilipata nafasi ya kucheza na Everton baada ya kuibuka bingwa wa michuano ya SportPesa Super Cup 2017, ikiwafunga mahasimu, AFC Leopatrds 3-0.

Timu nane zilishiriki michuano hiyo ya wiki moja Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam – mbali na Gor Mahia na Leopards, nyingine ni Tusker na Nakuru All Stars za Kenya pia, Jang’ombe Boys ya Zanzibar, Simba SC, Yanga SC na Singida Unted za Tanzania.

Wenyeji Simba SC na Yanga SC hawakufika mbali kwa sababu wiki ya michuano hiyo wachezaji wao wengi nyota walikuwa kwenye vikosi mbalimbali vya timu za taifa na kujikuta wakitumia wachezaji wengi wa akiba na wa timu za vijana. Post Bottom Ad