Kamanda Mpinga awa RPC mpya Mkoa wa Mbeya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 14, 2017

Kamanda Mpinga awa RPC mpya Mkoa wa Mbeya.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro, amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari.

 Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu.

Aidha, Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (DCP) Dhahiri Kidavashari amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi.

Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji wa kazi za Polisi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.

Imetolewa na:
Barnabas D. Mwakalukwa – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Post Bottom Ad