Rais wa TFF Jamal Malinzi na wenzake kuendelea kusota Rumande. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 03, 2017

Rais wa TFF Jamal Malinzi na wenzake kuendelea kusota Rumande.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewanyima dhamana Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa kwa kesi inayowakabili kwa sababu baadhi ya makosa wanayo tuhumiwa nayo (utakatishaji fedha) hayana dhamana.

 Kesi imeahirishwa hadi Julai 17, 2017. Kwa maana hiyo Malinzi na wenzake wanarudishwa tena rumande hadi tarehe iliyotajwa kusikiliza shauri lao.
Mawakili wa upande wa utetezi wakiongozwa na James Bwana waliiomba mahakama iwafikirie dhamana wateja wao kwa kutumia vifungu vya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambavyo vinasema kwamba, mtuhumiwa anaonekana hana hatia mpaka pale itakapothibitishwa na mahakama.

Upande wa mashtaka kwa kutumia pia vifungu vya sheria ambavyo vinasema makosa ya utakatishaji fedha hayana dhamana hivyo wakaishauri mahakama kutotoa dhamana kwa watuhumiwa wote.

Upande wa mahakama haijakubaliana na upande wa utetezi, mahakama imewanyima dhamana watuhumiwa wote na kuiahirisha kesi hiyo hadi Julai 27, 2017.

Malinzi na Mwesigwa walishikwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mnamo Juni 27 kwa kutuhumiwa matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao na kupandishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Juni 29 na kusomewa mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad